Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 119

Zaburi 119:71-97

Help us?
Click on verse(s) to share them!
71Ni vizuri kwangu kuwa nimeteseka ili niweze kujifunza sheria zako.
72Maagizo yatokayo kinywani mwako ni ya thamani zaidi kwangu kuliko maelfu ya vipande vya dhahabu na fedha. YOD.
73Mikono yako imeniumba na kunitengeneza; unipe uelewa ili niweze kujifunza amri zako.
74Wale wanao kucha wewe watafurahi wanionapo kwa sababu ninapata tumaini katika neno lako.
75Ninajua, Yahwe, kuwa amri zako ni za haki, na kuwa katika uaminifu ulinitesa.
76Agano lako aminifu na linifariji, kama ulivyomwahidi mtumishi wako.
77Unihurumie ili niweze kuishi, kwa maana sheria yako ni furaha yangu.
78Wenye kiburi na waaibishwe, maana wamenitukana; bali mimi nitayatafakari maagizo yako.
79Wale wote wanao kucha wewe na wanigeukie, wale wazijuao amri za agano lako.
80Moyo wangu uwe mkamilifu pamoja na heshima kwa sheria zako ili nisiaibike. KAPH.
81Ninazimia kwa kutamani sana kuwa wewe unaweza kuniokoa! Ninamatumaini katika neno lako.
82Macho yangu yanatamani sana kuiona ahadi yako; ni lini utanifariji mimi?
83Kwa maana nimekuwa kama kiriba katika moshi; sisahau sheria zako.
84Ni kwa muda gani gani mtumishi wako atalazimika kuyavumilia haya; ni lini utawahukumu wale wanaonitesa?
85Wenye kiburi wamenichimbia shimo, wasiotii sheria yako.
86Amri zako zote ni za kuaminika; wale watu walinitesa bila ya haki; unisaidie.
87karibu kunifanya nifikie mwisho juu ya nchi hii, lakini siyakatai maagizo yako.
88Kwa upendo wako thabiti, uniweke hai, ili niweze kuzitii amri zako. LAMEDH.
89Yahwe, neno lako linasimama milele; neno lako limefanywa imara mbinguni.
90Uaminifu wako wadumu kwa ajili ya vizazi vyote; umeiimarisha nchi, nayo inadumu.
91Vitu yote yaliendelea mpaka leo hii, kama vile ulivyosema katika amri zako za haki, maana vitu vyote ni watumishi wako.
92Kama sheria yako isingekuwa furaha yangu, ningeangamia katika mateso yangu.
93Sitayasahau kamwe maagizo yako, maana kupitia hayo umeniweka hai.
94Mimi ni wako, kwa maana ninayatafuta maagizo yao.
95Waovu hujiandaa kuniangamiza, lakini nitatafuta kuzielewa amri za agano lako.
96Nimeona kuwa kila kitu kina mipaka, lakini amri zako ni pana, zaidi ya mipaka. MEM.
97Oh ni jinsi gani naipenda sheria yako! Ni tafakari yangu mchana kutwa.

Read Zaburi 119Zaburi 119
Compare Zaburi 119:71-97Zaburi 119:71-97