Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 119

Zaburi 119:68-83

Help us?
Click on verse(s) to share them!
68Wewe ni mwema, na ndiye yule utendaye mema; unifundishe sheria zako.
69Wenye kiburi wamenichafua kwa uongo, lakini niliyashika maagizo yako kwa moyo wangu wote.
70Mioyo yao ni migumu, lakini ninafurahia katika sheria yako.
71Ni vizuri kwangu kuwa nimeteseka ili niweze kujifunza sheria zako.
72Maagizo yatokayo kinywani mwako ni ya thamani zaidi kwangu kuliko maelfu ya vipande vya dhahabu na fedha. YOD.
73Mikono yako imeniumba na kunitengeneza; unipe uelewa ili niweze kujifunza amri zako.
74Wale wanao kucha wewe watafurahi wanionapo kwa sababu ninapata tumaini katika neno lako.
75Ninajua, Yahwe, kuwa amri zako ni za haki, na kuwa katika uaminifu ulinitesa.
76Agano lako aminifu na linifariji, kama ulivyomwahidi mtumishi wako.
77Unihurumie ili niweze kuishi, kwa maana sheria yako ni furaha yangu.
78Wenye kiburi na waaibishwe, maana wamenitukana; bali mimi nitayatafakari maagizo yako.
79Wale wote wanao kucha wewe na wanigeukie, wale wazijuao amri za agano lako.
80Moyo wangu uwe mkamilifu pamoja na heshima kwa sheria zako ili nisiaibike. KAPH.
81Ninazimia kwa kutamani sana kuwa wewe unaweza kuniokoa! Ninamatumaini katika neno lako.
82Macho yangu yanatamani sana kuiona ahadi yako; ni lini utanifariji mimi?
83Kwa maana nimekuwa kama kiriba katika moshi; sisahau sheria zako.

Read Zaburi 119Zaburi 119
Compare Zaburi 119:68-83Zaburi 119:68-83