33Unifundishe, Yahwe, njia za sheria yako, nami nitazishika hadi mwisho.
34Unipe uelewa, nami nitazishika sheria zako; nitazitii kwa moyo wangu wote.
35Uniongoze katika njia ya amri zako, maana ninafurahi kuenenda katika hizo.
36Uelekeze moyo wangu kuzielekea amari za agano lako na uniweke mbali na matendo yasiyo haki tena.
37Uyageuze macho yangu dhidi ya kutazama mambo yasiyofaa; unihuishe katika njia zako.
38Umtendee mtumishi wako ahadi ambayo uliifanya kwa wale wanaokuheshimu wewe.
39Uniondolee shutumu niiogopayo, maana hukumu zako za haki ni njema.
40Tazama, nimeyatamani maagizo yako; unihuishe katika haki yako. VAV.
41Ee Yahwe, unipe upendo wako usiokwisha na wokovu wako kulingana na ahadi yako;
42ndipo nitakuwa na jibu kwa ajili ya yule anayenidhihaki.
43Usiliondoe neno la kweli mdomoni mwangu, maana nimesubiri kwa ajili ya amri zako za haki.