144Amri za agano lako ni za haki milele; unipe uelewa ili niweze kuishi. QOPH.
145Nililia kwa moyo wangu wote, “Unijibu, Yahwe, nitazishika sheria zako.
146Ninakuita wewe; uniokoe, nami nitazitii amri za agano lako.”
147NInaamka asubuhi kabla jua halijachomoza na kulia kwa ajili ya msaada.
148Ninatumaini katika maneno yako. Macho yangu yako wazi usiku kucha ili niweze kutafakari juu ya neno lako.
149Sikia sauti yangu katika uaminifu wa agano lako; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika amri zako za haki.
150Wale wanaonitesa wananikaribia, lakini wako mbali na sheria yako.
151Wewe uko karibu, Yahwe, na amri zako ni za kuaminika.
152Muda mrefu uliopita nilijifunza kutoka katika amri za agano lako ulizoziweka katika mahali pa milele. RESH.
153Uyatazame mateso yangu na unisaidie, maana siisahau sheria yako.
154Unitetee na kunikomboa; unihifadhi, kama ulivyo ahidi katika neno lako.
155Wokovu uko mbali na waovu, maana hawazipendi amri zako.