Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 119

Zaburi 119:137-174

Help us?
Click on verse(s) to share them!
137Wewe ni mwenye haki, Yahwe, na amri zako ni haki.
138Umezipa amri za agano lako haki na uaminifu.
139Hasira imeniangamiza kwa sababu adui zangu husahau maneno yako.
140Neno lako limepimwa sana, naye mtumishi wako analipenda.
141Sina umuhimu na ninadharauliwa, lakini bado siyasahau maagizo yako.
142Hukumu yako ni ya haki milele, na sheria yako ni ya kuaminika.
143Japo dhiki na taabu vimenipata, amri zako bado ni furaha yangu.
144Amri za agano lako ni za haki milele; unipe uelewa ili niweze kuishi. QOPH.
145Nililia kwa moyo wangu wote, “Unijibu, Yahwe, nitazishika sheria zako.
146Ninakuita wewe; uniokoe, nami nitazitii amri za agano lako.”
147NInaamka asubuhi kabla jua halijachomoza na kulia kwa ajili ya msaada.
148Ninatumaini katika maneno yako. Macho yangu yako wazi usiku kucha ili niweze kutafakari juu ya neno lako.
149Sikia sauti yangu katika uaminifu wa agano lako; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika amri zako za haki.
150Wale wanaonitesa wananikaribia, lakini wako mbali na sheria yako.
151Wewe uko karibu, Yahwe, na amri zako ni za kuaminika.
152Muda mrefu uliopita nilijifunza kutoka katika amri za agano lako ulizoziweka katika mahali pa milele. RESH.
153Uyatazame mateso yangu na unisaidie, maana siisahau sheria yako.
154Unitetee na kunikomboa; unihifadhi, kama ulivyo ahidi katika neno lako.
155Wokovu uko mbali na waovu, maana hawazipendi amri zako.
156Matendo yako ya huruma ni makuu, Yahwe; uniweke hai; kama ufanyavyo siku zote.
157Watesi wangu na adui zangu ni wengi, lakini bado sijaenda mbali na amri za agano lako.
158Nimewaona wasaliti wakitia kinyaa kwa sababu hawalishiki neno lako.
159Tazama jinsi niyapendavyo maagizo yako; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika uaminifu wa agano lako.
160Kiini cha neno lako ni kweli; kila mmoja mwenye amri za haki hudumu milele. SHIN.
161Wakuu hunitesa bila sababu; moyo wangu hutetemeka, ukiogopa kutolitii neno lako.
162Ninalifurahia neno lako kama apataye nyara nyingi.
163Ninachukia na kudharau uongo, lakini naipenda sheria yako.
164Mara saba kwa siku ninakusifu wewe kwa sababu ya amri zako za haki.
165Wana amani nyingi, waipendao sheria yako; hakuna cha kuwatia mashakani.
166Naungoja wokovu wako, Yahwe, na ninatii amri zako.
167Ninazishika amri zako thabiti, na ninazipenda sana.
168Ninayashika maagizo yako na amri zako thabiti, kwa maana unajua kila kitu nifanyacho. TAV.
169Sikia kilio changu, Yahwe; unipe uelewa wa neno lako.
170Maombi yangu yaje mbele zako; unisaidie, kama ulivyoahidi katika neno lako.
171Midomo yangu na imwage sifa, maana wewe unanifundisha sheria zako.
172Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, maana amri zako zote ni za haki.
173Mkono wako unisaidie, maana nimechagua maagizo yako.
174Ninautamani wokovu wako, Yahwe, na sheria yako ni furaha yangu.

Read Zaburi 119Zaburi 119
Compare Zaburi 119:137-174Zaburi 119:137-174