130Ufafanuzi wa maneno yako huleta nuru; na kumpa ufahamu mjinga.
131Ninafungua kinywa changu na kutweta, maana ninazitamani amri zako.
132Unigeukie na unihurumie, kama ufanyavyo siku zote kwa wale walipendao jina lako.
133Uziongoze hatua zangu kwa neno lako; usiruhusu dhambi yeyote initawale.
134Unikomboe dhidi ya wanadamu waonevu ili niyatii maagizo yako.
135Uso wako umwangazie mtumishi wako, na unifundishe sheria zako.
136Mito ya machozi yatiririka kutoka machoni pangu kwa sababu watu hawaitii sheria yako. TSADHE.
137Wewe ni mwenye haki, Yahwe, na amri zako ni haki.
138Umezipa amri za agano lako haki na uaminifu.