128Hivyo ninayafuata maagizo yako yote kwa makini, na ninachukia kila njia ya uongo. PE.
129Sheria zako ni za ajabu, ndiyo sababu ninazitii.
130Ufafanuzi wa maneno yako huleta nuru; na kumpa ufahamu mjinga.
131Ninafungua kinywa changu na kutweta, maana ninazitamani amri zako.
132Unigeukie na unihurumie, kama ufanyavyo siku zote kwa wale walipendao jina lako.
133Uziongoze hatua zangu kwa neno lako; usiruhusu dhambi yeyote initawale.
134Unikomboe dhidi ya wanadamu waonevu ili niyatii maagizo yako.
135Uso wako umwangazie mtumishi wako, na unifundishe sheria zako.