115Ondokeni kwangu, ninyi mtendao uovu, ili niweze kuzitii amri za Mungu wangu.
116Uniwezeshe kwa neno lako ili niweze kuishi na nisiaibike na matumaini yangu.
117Unisaidie, nami nitakuwa salama; siki zote nitazitafakari sheria zako.
118Wewe huwakataa wale wote wapoteao mbali na sheria zako, maana watu hao ni wadanganyifu na si wakuaminika.
119Wewe huwaondoa waovu wa nchi kama takataka; kwa hiyo ninazipenda amri zako thabiti.
120Mwili wangu hutetemeka kwa hofu yako, na ninaziogopa amri za haki yako. AYIN.
121Ninafanya kilicho sahihi na haki; usiniache kwa watesi wangu.
122Uwe mdhamini wa ustawi wa mtumishi wako; usiwaache wenye kiburi wanionee.
123Macho yangu yanachoka kwa kuusubiri wokovu wako na neno lako la haki.
124Mwoneshe mtumishi wako uaminifu wa agano lako, na unifundishe sheria zako.
125Mimi ni mtumishi wako; unipe uelewa ili niweze kuzijua amri za agano lako.
126Ni wakati wa Yahwe kutenda, kwa maana watu wamevunja sheria yako.