Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 119

Zaburi 119:107-140

Help us?
Click on verse(s) to share them!
107Nimeteswa sana; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika neno lako.
108Yahwe, tafadhali pokea dhabihu yangu ya hiari ya kinywa changu, na unifundishe amri zako za haki.
109Uhai wangu ziku zote uko mkononi mwangu, lakini bado sisahau sheria yako.
110Waovu wamenitegea mtego, lakini sijapotea mbali na maagizo yako.
111Nimezifanya amri za agano lako kama urithi wangu milele, maana hizo ni furaha ya moyo wangu.
112Moyo wangu umewekwa kuzitii sheria zako milele mpaka mwisho kabisa. SAMEKH.
113Ninawachukia watu wa kusita-sita, lakini naipenda sheria yako.
114Wewe ni ficho langu na ngao yangu; nalingoja neno lako.
115Ondokeni kwangu, ninyi mtendao uovu, ili niweze kuzitii amri za Mungu wangu.
116Uniwezeshe kwa neno lako ili niweze kuishi na nisiaibike na matumaini yangu.
117Unisaidie, nami nitakuwa salama; siki zote nitazitafakari sheria zako.
118Wewe huwakataa wale wote wapoteao mbali na sheria zako, maana watu hao ni wadanganyifu na si wakuaminika.
119Wewe huwaondoa waovu wa nchi kama takataka; kwa hiyo ninazipenda amri zako thabiti.
120Mwili wangu hutetemeka kwa hofu yako, na ninaziogopa amri za haki yako. AYIN.
121Ninafanya kilicho sahihi na haki; usiniache kwa watesi wangu.
122Uwe mdhamini wa ustawi wa mtumishi wako; usiwaache wenye kiburi wanionee.
123Macho yangu yanachoka kwa kuusubiri wokovu wako na neno lako la haki.
124Mwoneshe mtumishi wako uaminifu wa agano lako, na unifundishe sheria zako.
125Mimi ni mtumishi wako; unipe uelewa ili niweze kuzijua amri za agano lako.
126Ni wakati wa Yahwe kutenda, kwa maana watu wamevunja sheria yako.
127Hakika ninazipenda amri zako kuliko dhahabu, naam, kuliko dhahabu safi.
128Hivyo ninayafuata maagizo yako yote kwa makini, na ninachukia kila njia ya uongo. PE.
129Sheria zako ni za ajabu, ndiyo sababu ninazitii.
130Ufafanuzi wa maneno yako huleta nuru; na kumpa ufahamu mjinga.
131Ninafungua kinywa changu na kutweta, maana ninazitamani amri zako.
132Unigeukie na unihurumie, kama ufanyavyo siku zote kwa wale walipendao jina lako.
133Uziongoze hatua zangu kwa neno lako; usiruhusu dhambi yeyote initawale.
134Unikomboe dhidi ya wanadamu waonevu ili niyatii maagizo yako.
135Uso wako umwangazie mtumishi wako, na unifundishe sheria zako.
136Mito ya machozi yatiririka kutoka machoni pangu kwa sababu watu hawaitii sheria yako. TSADHE.
137Wewe ni mwenye haki, Yahwe, na amri zako ni haki.
138Umezipa amri za agano lako haki na uaminifu.
139Hasira imeniangamiza kwa sababu adui zangu husahau maneno yako.
140Neno lako limepimwa sana, naye mtumishi wako analipenda.

Read Zaburi 119Zaburi 119
Compare Zaburi 119:107-140Zaburi 119:107-140