Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 119

Zaburi 119:105-111

Help us?
Click on verse(s) to share them!
105Neno lako ni taa ya mguu miguu yangu na mwanga wa njia yangu.
106Nimeapa na nimethibitisha, kuwa nitazitii amri za haki yako.
107Nimeteswa sana; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika neno lako.
108Yahwe, tafadhali pokea dhabihu yangu ya hiari ya kinywa changu, na unifundishe amri zako za haki.
109Uhai wangu ziku zote uko mkononi mwangu, lakini bado sisahau sheria yako.
110Waovu wamenitegea mtego, lakini sijapotea mbali na maagizo yako.
111Nimezifanya amri za agano lako kama urithi wangu milele, maana hizo ni furaha ya moyo wangu.

Read Zaburi 119Zaburi 119
Compare Zaburi 119:105-111Zaburi 119:105-111