Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 93

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahwe anatawala; amevikwa adhama; Yahwe amejivika na kujifunga nguvu. Ulimwengu umeimalishwa; hauwezi kusogezwa.
2Kiti chako cha enzi kimeimarishwa nyakati za kale; umekuwepo siku zote.
3Bahari zimeinuka, Yahwe; zimemepaza sauti zao; mawimbi ya bahari yapiga ghasia na ngurumo.
4Zaidi ya ghasia ya mawimbi mengi, mawimbi ya bahari yenye nguvu, Yahwe aliye juu ni mwenye nguvu.
5Amri zako makini ni za kuaminika sana; utakatifu huipamba nyumba yako, Yahwe, milele.