Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 135

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Msifuni Yahwe. Lisifuni jina la Yahwe. Msifuni yeye, enyi watumishi wa Yahwe,
2ninyi msimamao katika nyumba ya Yahwe, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.
3Msifuni Yahwe, kwa kuwa ni mwema; liimbieni sifa jina lake, maana ni vizuri kufanya hivyo.
4Kwa kuwa Yahwe amemchagua Yakobo kwa ajili yake mwenyewe, Israeli kama urithi wake.
5Najua ya kuwa Yahwe ni mkuu, na kwamba Bwana wetu yuko juu ya miungu yote.
6Chochote Yahwe apendacho, hufanya mbinguni, duniani, katika bahari na katika vilindi vyote.
7Hushusha mawingu kutoka mbali, akifanya mianga ya radi kuongozana na mvua na kuleta upepo toka katika ghala yake.
8Aliua mzaliwa wa kwanza wa Misri, wote wanadamu na wanyama.
9Alituma ishara na maajabu kati yako Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote.
10Aliwashambulia mataifa mengi na aliua wafalme wenye nguvu,
11Sihoni mfalme wa Waamori na Ogu mfalme wa Bashani na falme zote za Kanaani.
12Alitupatia sisi nchi yao kama urithi, urithi wa Israeli watu wake.
13Jina lako, Yahwe, inadumu milele; Yahwe, kumbukumbu lako vizazi hata vizazi.
14Kwa kuwa Bwana huwatetea watu wake na anahuruma juu ya watumishi wake.
15Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu.
16Sanamu hizo zina vinywa, lakini haziongei; zina macho, lakini hazioni;
17zina masikio, lakini hazisikii, wala vinywani mwao hamna pumzi.
18Wale wazitengenezao wanafanana nazo, vilevile kila anaye zitumainia.

19Enyi kizazi cha Israeli, mtukuzeni Yahwe; kizazi cha Haruni, mtukuzeni Yahwe.
20Kizazi cha Lawi, mtukuzeni Yahwe.
21Atukuzwe Yahwe katika Sayuni, yeye aishiye Yerusalemu. Msifuni Yahwe.