Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Luka - Luka 18

Luka 18:37-43

Help us?
Click on verse(s) to share them!
37Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.”
38Naye akapaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”
39Wale watu waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze; lakini yeye akazidi kupaza sauti: “Mwana wa Daudi, nihurumie;”
40Yesu alisimama, akaamuru wamlete mbele yake. Yule kipofu alipofika karibu, Yesu akamwuliza,
41“Unataka nikufanyie nini?” Naye akamjibu, “Bwana, naomba nipate kuona tena.”
42Yesu akamwambia, “Ona! Imani yako imekuponya.”
43Na mara yule aliyekuwa kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.

Read Luka 18Luka 18
Compare Luka 18:37-43Luka 18:37-43