Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 18

Luka 18:37-43

Help us?
Click on verse(s) to share them!
37Wakamwambia kwamba Yesu wa Nazareti anapita.
38Hivyo yule kipofu akalia kwa sauti, akisema, 'Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.'
39wale waliokuwa wakitembea walimkemea huyo kipofu, wakamwambia anyamaze. Lakini yeye akazidi kulia kwa sauti, 'Mwana wa Daudi, unirehemu.
40Yesu akasimama akaamuru mtu yule aletwe kwake. Kisha yule kipofu alipomkaribia, Yesu akamwuliza,
41'Unataka nikufanyie nini?' Akasema, 'Bwana, nataka kuona.'
42Yesu akamwambia, 'Upate kuona. Imani yako imekuponya.'
43Mara hiyo akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Walipoona hili, watu wote wakamsifu Mungu.

Read Luka 18Luka 18
Compare Luka 18:37-43Luka 18:37-43