Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 18:37-43 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 18:37-43 in Biblia Takatifu

37 Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.”
38 Naye akapaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”
39 Wale watu waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze; lakini yeye akazidi kupaza sauti: “Mwana wa Daudi, nihurumie;”
40 Yesu alisimama, akaamuru wamlete mbele yake. Yule kipofu alipofika karibu, Yesu akamwuliza,
41 “Unataka nikufanyie nini?” Naye akamjibu, “Bwana, naomba nipate kuona tena.”
42 Yesu akamwambia, “Ona! Imani yako imekuponya.”
43 Na mara yule aliyekuwa kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.
Luka 18 in Biblia Takatifu

Luka 18:37-43 in Biblia ya Kiswahili

37 Wakamwambia kwamba Yesu wa Nazareti anapita.
38 Hivyo yule kipofu akalia kwa sauti, akisema, 'Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.'
39 wale waliokuwa wakitembea walimkemea huyo kipofu, wakamwambia anyamaze. Lakini yeye akazidi kulia kwa sauti, 'Mwana wa Daudi, unirehemu.
40 Yesu akasimama akaamuru mtu yule aletwe kwake. Kisha yule kipofu alipomkaribia, Yesu akamwuliza,
41 'Unataka nikufanyie nini?' Akasema, 'Bwana, nataka kuona.'
42 Yesu akamwambia, 'Upate kuona. Imani yako imekuponya.'
43 Mara hiyo akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Walipoona hili, watu wote wakamsifu Mungu.
Luka 18 in Biblia ya Kiswahili