Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 4

Luka 4:9-32

Help us?
Click on verse(s) to share them!
9Baadaye Ibilisi alimwongoza Yesu hadi Yerusalemu na kumweka sehemu ya juu kabisa ya jengo la hekalu na kumwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa.
10Kwa sababu imeandikwa, “Atawaagiza malaika zake wakutunze na kukulinda,
11na watakuinua juu mikononi mwao ili kwamba usiumize miguu yako juu ya jiwe.”
12Yesu akijibu alimwambia, “Imenenwa, “usimjaribu Bwana Mungu wako.”
13Ibilisi alipomaliza kumjaribu Yesu, alienda zake na kumwacha hadi wakati mwingine.
14Kisha Yesu alirudi Galilaya kwa nguvu za Roho, na habari kumhusu yeye zikaenea na kusambaa katika mikoa jirani yote.
15Alifundisha katika masinagogi yao, na kila mmoja alimsifu.
16Siku moja alikwenda Nazareti, mji ambao alilelewa na kukulia. Kama ilivyokuwa desturi yake aliingia kwenye sinagogi siku ya sabato, na alisimama kusoma maandiko.
17Alikabidhiwa gombo la nabii Isaya, hivyo, alilifungua gombo na akatafuta sehemu iliyoandikwa,
18“Roho wa Bwana yuu juu yangu, kwa sababu alinitia mafuta kuhubiri habari njema kwa maskini. Amenituma kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kuwafanya wasioona waweze kuona tena. Kuwaweka huru wale wanaogandamizwa,
19kuutangaza mwaka ambao Bwana ataonesha wema wake.”
20Kisha akalifunga gombo, akamrudishia kiongozi wa sinagogi, na akaketi chini. Macho ya watu wote waliokuwa katika sinagogi yalimwangalia yeye.
21Alianza kuzungumza nao akisema, “Leo andiko hili limetimizwa masikioni mwenu.”
22Kila mmoja pale alishuhudia kile alichokisema Yesu, na wengi miongoni mwao walishangazwa na maneno ya hekima yaliyokuwa yakitoka katika kinywa chake. Walikuwa wakisema, “huyu ni kijana tu wa Yusufu, siyo hivyo?”
23Yesu akawaambia, “hakika mtasema methali hii kwangu, “Tabibu, jiponye mwenyewe. Chochote tulichosikia ukifanya Kapernaumu, kifanye hapa pia kijijini kwako.”
24Pia alisema, “hakika nawaambia ninyi, hakuna nabii anayekubalika katika nchi yake.”
25Lakini nawaambia ninyi kweli kwamba kulikuwa na wajane wengi Israel katika kipindi cha Eliya, wakati mbingu ilipofungwa kusiwe na nvua kwa miaka mitatu na nusu, wakati kulipokuwa na njaa kubwa katika nchi yote.
26Lakini Eliya hakutumwa kwa yeyote mmoja wao, lakini kwa mjane mmoja tu aliyeishi Sarepta karibu na mji wa Sidoni.
27Pia, kulikuwa na wakoma wengi Israel katika kipindi cha Elisha nabii, lakini hakuna hatammoja wao aliyeponywa isipokuwa Naamani mtu wa Siria.
28Watu wote ndani ya sinagogi walijawa na gadhabu walipoyasikia haya yote.
29Walisimama na kumsukumizia nje ya mji, na kumwongoza mpaka kwenye ukingo wa mlima wa mji ambapo mji wao ulijengwa juu yake, ili waweze kumtupa chini.
30Lakini alipita salama katikati yao na akaenda zake.
31Kisha alitelemkia Kapernaumu, katika mji wa Galilaya. Sabato moja alikuwa akifundisha watu ndani ya sinagogi.
32Walishangazwa na mafundisho yake, kwasababu alifundisha kwa mamlaka.

Read Luka 4Luka 4
Compare Luka 4:9-32Luka 4:9-32