Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu

Hesabu 33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Hizi ndizo safari za wana wa Israeli hapo walipotoka katika nchi ya Misri pamoja na makundi yao ya kijeshi chini ya uongozi wa Musa na Haruni.
2Musa aliandika maeneo yote tangu walipoondoka mpaka walipofika, kama alivyoamuriwa na BWANA. Hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa kwa kila walipotoka.
3Mwezi wa kwanza walisafiri kutoka Ramesi, waliondoka siku ya kumi na tano. Asubuhi siku iliyofuata baada ya Pasaka, Wana wa Israeli waliondoka wazi wazi, mbele ya machoya Wamisri wote.
4Hii ilitokea wakati Wamisiri walipokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza, ambao BWANA alikuwa amewaua miongoni mwao, kwa kuwa pia alikuwa ameiadhibu miungu yao.
5Wana wa Israeli walisafiri kutoka Ramesi na kuweka kambi
6Sukothi. Walisafiri toka Sukothi na kuweka kambi Ethamu, mwisho wa nyika.
7Wakasafiri kutoka Ethamu wakarudi mpaka Pi-Hahirothi, ambayo inaikabili Baali Zephoni, ambapo waliweka kambi kuikabili Migidoli
8Kisha wakasafiri toka mkabala wa Pi-Hairothi na kupita katikati ya bahari kuelekea nyikani. Wakasafiri safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu na kuweka kambi Mara.
9Wakasafiri kutoka Mara kufika Elimu. Pale Elimu kulikuwa na chemichemi kumi na mbili za maji na miti sabini ya mitende. hapo ndipo walipoweka kambi.
10Walisafiri kutoka Elimu na kuweka kambi karibu na Bahari ya Shamu.
11Walisafiri kutoka Bahari ya Shamu na kuweka kambi katika nyika ya Sini.
12Walisafiri kutoka nyika ya Sini na kuweka kambi Dofka.
13Wakasafiri kutoka Dofka na kuweka kambi Alushi.
14Wakasafiri kutoka Alushi na kuweka kambi Refidimu, ambapo watu walikosa maji ya kunywa.
15Walisafiri kutoka Refidimu na kuweka kambi kwenye nyika ya Sinai.
16Walisafiri kutoka nyika ya Sinai na kuweka kambi Kibrothi Hataava.
17Walisafiri kutoka Kibrothi Hataava na kuweka kambi Hazerothi.
18Walisafiri kutoka Hazerothi na kuweka kambi Rithima.

19Walisafiri kutoka Rithima na kuweka kambi Rimoni Perezi.
20Walisafiri kutoka Rimoni Perezi na kuweka kambi Libna.
21Walisafiri kutoka Libna na kuweka kambi Risa.
22Walisafiri kutoka Risa na kuweka kambi Kehelatha.
23Walisafiri kutoka Kehelatha na kuweka kambi kwenye Mlima Sheferi.
24Walisafiri kutoka Mlima Sheferi na kuweka kambi Harada.
25Walisafiri kutoka Harada na kuweka kambi Makelothi.
26Walisafiri kutoka Makelothi na kuweka kambi Tahathi.
27Walisafiri kutoka Ttahalathi na kuweka kambi Tera.
28Walisafiri kutokaTera na kuweka kambi Mithika.
29Walisafiri kutoka Mithika na kuweka kambi Hashimona.
30Walisafiri kutoka Hashimona na kuweka kambi Moserothi.
31Walisafiri kutoka Moserothi na kuweka kambi Bene Jaakani.
32Walisafiri kutoka Bene Jaakani na kuweka kambi Hori Hagidigadi.
33Walisafiri kutoka Hori Hagidigadi na kuweka kambi Jotibatha.
34Walisafiri kutoka Jotibatha na kuweka kambi Abrona.
35Walisafiri kutoka Abrona na kuweka kambi Ezioni Geberi.
36Walisafiri toka Ezioini Geberi na kuweka kambi katika nyika ya Sini kule Kadeshi.

37Walisafiri kutoka Kadeshi na kuweka kambi Mlima Hori, Pembezoni mwa nchi ya Edomu.
38Hapo ndipo Haruni kuhani alipoenda kwenye Mlima Hori kwa amri ya BWANA na kufa kule mwaka wa arobaini bada ya Wisraeli kutoka katika nchi ya Misri, katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano.
39Haruni alikuwa na umri wa mika 123 alipokufa pale juu ya Mlima Hori.
40Wakanaani, mfalme wa Aradi, ambao waliishi kusini mwa nyika katika nchi ya Kanaani, walisikia juu ya ujio wa wana wa Israeli.
41Walisafiri kutika Mlima Hori n a kuweka kambi Zalimona.
42Walisafiri kutoka Zalimona na kuweka kambi Punoni.
43Walisafiri kutoka Punoni na kuweka kambi Obothi.
44Walisafiri kutoka Obothi na kuweka kambi Abarimu, katika mpaka wa Moabu.
45Walisafiri kutoka Abarimu na kuweka kambi Diboni Gadi.
46Walisafiri kutoka Diboni Gadi na kuweka kambi Alimoni Diblathaimu.
47Walisafiri kutoka Alimoni Diblathaimu na kuweka kambi kwenye milima ya Abarimu mkabala na Nebo.
48Walisafiri kutoka mlima wa Abarimuna kuweka kambi kwenye nyanda za Moabu karibu na Yorodani huko Yeriko.
49Waliweka kambi karibu na Yorodani, kutoka Bethi Jeshimothi mpaka Abeli Shitimu katika nyanda za Moabu.
50Hapo BWANA alinenana Musa katika nyanda za Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko akasema,
51“Nena na wana wa Israeli uwaambie. 'Mtakapovuka mto Yorodani kuingia Kanaani,
52ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote mbele yenu. Mtaziharibu sanamu zote za kuchongwa. Mtaziharibu sanamu zao za kusubu na kuharibu mahali pao pote palipoinuka.
53Mtachukua hiyo ardhi iwe mali yenu na muishi ndani yake, kwa sababu nimewapeni hiyo nchi iwe mali yenu.
54Mtairithi hiyo nchi kwa kupiga kura, kwa kufuata kila ukoo. Kwa zile koo kubwa kubwa mtawapa sehemu kubwa ya ardhi, na kwa zile koo ndogo ndogo mtawapa sehemu ndogo ya ardhi. Kura itakapoanguka kwenye kila ukoo, hiyo ardhi itakuwa mali yake. Mtairithi ardhi kufuata ukoo wa kabilla la jamaa zenu.

55Lakini kama hamtawafukuza wenyeji wa nchi hiyo watoke mbele yenu, ndipo wale watu mtakaowaruhusu wakae nanyi watakapokuwa kama sindano machoni mwenu na miiba katika mbavu zenu. Watayafanya maisha yenu yawe magumu katika nchi mnayoishi.
56Ndipo itakapotokea kuwa kile ambacho Mimi ninakusudia kufanya kwa wale watu, Nitawafanyia pia ninyi'”