Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu

Hesabu 7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Siku ambayo Musa alikamilsha masikani, alitia mafuta na kuiweka wakfu kwa BWANA, pamoja na mapambo yake. Aliifanyia hivyo madhabahu na vyombo vyake. Aliitia mafuta na kuiweka wakfu kwa BWANA.
2Siku hiyo, viongozi wa Israeli na wale vichwa vya familia za mababu walitoa sadaka. Hawa wanaume walikuwa viongozi wa makabila. Walisaidia kuhesabu watu kwenye ile sensa.
3Walileta sadaka zao kwa BWANA. Walileta magari sita yaliyofunikwa na mafahari kumi na mbili. Walileta gari moja kwa kila viongozi wawili, kila kiongozi alileta fahari moja. Walileta vitu hivi mbele ya masikani.
4Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,
5“Uzipokee hizo sadaka kutoka kwao na uzitumie kwa matumizi ya kazi ya hema ya kukutania. Uwape hizo sadaka Walawi, kwa kila mmoja kadri ya uhitaji wa kazi yake.”
6Musa akayatwaa yale magari na mafahari. na kuwapatia Walawi.
7Aliwapa magari mawili na mafahari wanne wale wa uzao wa Gerishoni, kwa sababu ndivyo kazi yao ilivyohitaji.
8Aliwapatia uzao wa Merari magari manne na mafahari nane, chini ya uangalizi wa Ithamari mwana wa Haruni kuhani. Alifanya hivi kwa sababu ya uhitaji wa kazi yao.
9Lakini wale wa uzao wa Kohathi hakuwapa chochote kwa sababu wao waliangalia vitu vtakatifu amabvyo vilipaswa vibebwe mabagani mwao, siyo kwa magari.
10Viongozi walitoa bidhaa zo zingine kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu katika siku ile ambayo Musa aliitia mafuta madhabahu. Viongozi walitoa sadaka zao mbele ya madhabahu hiyo.
11BWANA akasema na Musa, “kila kiongozi atatoa sadaka kwa siku yake kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu.”
12Katika siku ya kwanza, Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila ya Yuda, alitoa sadaka yake.
13Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja ya fedha ambayo uzito wake ni shekeli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
14Pia alimpa unga wa dhahabu kiasi cha bakuli moja chenye uzani wa shekeli kumi kilichojaa ubani
15Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, kondoo dume mmoja na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
16Alitoa beberu kama kama sadaka ya hatia.
17Alitoa makisai mbili, kondoo waume watano, beberu watano na wanakondoo dume watano wenye umri wa mwaka mmoja mmoja, kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
18Siku ya pili, Nethanel mwana wa Zuari, kiongozi wa Isakari, alitoa sadaka yake.

19Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha ya uzito wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa sheli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Viyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa sadaka ya unga.
20Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzito wa shekeli kumi, iliyojaa ubani.
21Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo mmoja dume.
22Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
23Alitoa makisai wawili, Kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hiii likuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Zuari.
24Siku ya tatu, Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa uzao wa Zabuloni alitoa sadaka yake.
25Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. vyombo vyote hivi vilikuwa vimeja unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
26Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
27Alitoa sadaka ya fahari mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja.
28Alitoa beberu mmoja kama sadaka ya dhambi.
29Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja. kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana Heloni.
30Siku ya nne, Elizuri mwana wa shedeuri, kiongozi wa uzao wa Reubeni, alitoa sadaka yake.
31Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
32Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichoo jaa ubani.
33Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, mwanakondoo dume mmoja mchanga wa mwaka mmoja.
34Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
35Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Elizuri mwana wa Shedeuri.
36Siku ya tano, Shelumieli mwana wa Zurishadai, kiongozi wa uzao wa Simeoni, alitoa sadaka yake.

37Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekali 130 na bakuli mojala fedha lenye uzani wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
38Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, uliojaa ubani.
39Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, dume la kondoo, na dume la mwanakondoo la mwaka mmoja.
40Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
41Alitao maksai wawili, dume wawili wa kondoo, beberu watano, na dume watano wa wanakondoo wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka y amani. Hiindiyo iliyokuwa sadka ya Shelumei mwana wa Zurishadai.
42Siku ya sita, Eliasafu mwana wa Deuli, kiongozi wa uzao wa Gadi, alitoa sadaka yake.
43Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la shaba lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya unga.
44Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
45Alitoa sadaka ya kuteketezwa ya fahari changa, kondoo dume mmoja, na dume la mwanakondoo mmoja wa mwaka mmoja.
46Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
47Alitoa maksai wawili, dume watano wa kondoo, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deuli.
48Siku ya saba, Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa uzao wa Efraimu, alitoa sadaka yake.
49Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
50Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu, kilichojaa ubani
51Alitoa sadaka ya kuteketezwa, fahari mmoja, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
52Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
53Alitoa maksai wawili, kondo dume watano, beberu watano, na na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sdaka ya Elishama mwana wa Amidu.
54Siku y a nane, Gamaliel mwana wa Pedazuri, kiongozi wa uzao wa Manase, alitoa sadaka yake.

55Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
56Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
57Alitoa sadaka ya kuteketezwa ya fahari mmoja, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
58Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
59Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Gamaliel mwana wa Pedazuri.
60Siku ya tisa, Abidani mwana wa Gidioni, kiongozi wa uzao wa Benjamini, alitoa sadaka yake.
61Sadaka yake ilikuwa sahani moja yafedha yenye uzani wa sheli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
62Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
63Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
64Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
65Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Abidani mwana wa Gidioni.
66Siku ya kumi, Ahizeri mwana wa Amishadai kiongozi wa Dani alitoa sadaka yake.
67Alitoa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
68Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzito wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
69Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, dume moja la kondoo, na dume moja la mwanakondoo wa mwaka mmoja.
70Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
71Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja, kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahizeri mwana wa Amishadai.
72Siku ya kumi na moja. Pagieli mwana wa Okrani kiongozi wa uzao wa Asheri alaitoa sadaka yake.

73Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabani, kwa kipimo cha shekeli ya mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
74Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
75Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga. dume la kondoo moja, dume moja la mwanakondoo wa mwaka mmoja.
76Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
77Alitoa maksai wawili, dume watano wa kondoo, na wanakondoo dume watano kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.
78Siku ya kumi na mbili., Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa uzao wa Naftali, alitoa sadaka yake.
79Sadaka yake ailikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba ulichanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
80Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
81Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, dume moja la kondoo, na mwanakondoo dume moja wa mwaka mmoja.
82Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
83Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahra mwana wa Enani.
84Viongozi wa Israeli waliviweka wakfu hivi vitu vyote siku ambayo Musa alimimina mafuta kwenye madhabahu. Waliziweka wakfu zile sahani kumi na mbili za fedha, Bakuli kumi na mbili za fedha, na vijiko kumi na vili vya dhahabu.
85Zile sahani za fedha kila moja ilikuwa na uzani wa shaekeli 130 na kila bakuli ye fedha ilikuwa na uzani wa shekeli sabini. Vyombo vyote vya fedh vilikuwa na ujumla ya uzani wa shekeli 2, 400, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu.
86Vile vijiko vya dhahabu vilivyokuwa vimejaa ubani, vilikuwa na uzani wa shekeli kumi kila kimoja. Vijiko vyote vya dhahabu vilikuwa na uzani wa shekeli 120.
87Waliwatenga wanyama wote kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, fahari kumi na wawili, kondoo dume kumi na wawili, na wanakondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja mmoja. Walitoa sadaka yao ya unga. Walitoa beberu kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi.
88Kutokana na ng'ombe zao, walitoa fahari ishirini na nne, kondoo dume sitini beberu sitini, na wanakondoo dume sitini wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa kwa ajiliya kuiweka wafu ile madhabahu baada ya kumiminiwa mafuta.
89Musa alipoingia kwenye hema ya kukutania kusema na BWANA, ndipo alipoisikia sauti yake ikisema naye. BWANA alinena naye kutoka juu ya kiti cha rehema kilichokuwa juu ya sanduku la ushahidi, kutoka katikati ya makerubi. Alinena naye.