Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu

Hesabu 23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Balaamu akamwabia Balaki, “Jenga madhabahu saba kwa ajili yangu na uandae mafahari saba na kondoo dume saba.”
2Kwa hiyo Balaki akafanya kama Balaamu alivyoomba. Kisha Balaki na Balaamu wakatoa sadaka ya fahari mmoja na kondoo dume mmoja kwa kila madhabahu.
3Ndipo Balaamu alipomwamiba Balaki, “Simama kwenye sadaka yako ya kuteketezwa na mimi nitaenda. Labda BWANA atakuja kukutana na mimi. Chochote atakachoniambia nitakuambia.” Kwa hiyo akaenda juu ya mlima usiokuwa na miti.
4Wakati bado akiwa juu ya mlima. Mungu akakutana naye, na Balaamu akamwambia, “Nimejenga madhabahu saba, na nimetoa sadaka ya fahari na kondoo dume kwa kila madhabahu.”
5BWANA akaweka ujumbe kwenye kinywa cha Baalamu akasema, “Rudi kwa Balaki ukamwambie.”
6Kwa hiyo Balaamu akarudi kwa Balaki aliyekuwa amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na viongozi wote wa Moabu walikuwa pamoja naye.
7Ndipo Balaamu alipoanza kunena unabii wake akisema, “Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka katika milima ya mashariki, 'Njoo, nilaanie Yakobo kwa ajili yangu,' alisema, 'Njoo umtie unajisi Israeli,'
8Nawezaje kuwalaani wale ambao Mungu hajawalaani? Nawezaje kuwapinga wale ambao Mungu hawapingi?
9Kwa kuwa kutoka juu ya miamba Ninamwona; kutoka kwenye milima ninamtazama. Kuna watu wanaoishi pekee yao na hawajioni wenyewe kama ni taifa la kawaida.
10Nani awezaye kuyahesabu mavumbi ya Yakobo au kuhesabu hata robo ya Israeli? Naomba nife kifo cha mtu mwenye haki, na mwisho wa maisha yangu uwe kama wake!”
11Balaki akamwambia Balaamu, “Umenifanyia nini? Nilikuleta ili uwalaani maadui wangu, lakini ona, umewabariki,”
12Balaamu akajibu akasema, “Kwa nini nisiwe mwangalifu kusema kile ambacho BWANA anaweka kinywani mwangu?”
13Basi Balaki akamwambia, “Hebu uje nami kwenye eneo jingine ili uwaone. Utakaowaona ni wale wa karibu tu, huwezi kuwaona wote. Huko sasa unaweza kunilaania hawa watu.”
14Kwa hiyo akampeleka Balaamu kwenye shamba la Zofimu, lililo juu ya Mlima Pisiga, na kule akajenga madhabau zingine saba. Akatoa sadaka ya fahari mmoja na kondoo dume kwa kila madhabahu.
15Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Simama hapa karibu na sadaka zako, wakati mimi naenda kukutana na BWANA kule.”
16Kwa hiyo BWANA akakutana na Balaamu na kumwekea ujumbe kinywani mwake. Alimwambia, “Rudi kwa Balaki ukamwambie huu ujumbe toka kwangu.”
17Balaamu akamrudia, na tazama, alikuwa amesimama karibu na sadaka zake za kuteketezwa, na vionigozi wa Moabu walikuwa pamoja naye. Balaki akamwuliza, “BWANA amekwambiaje?”
18Balaamu akaanza kutoa unabii. Akasema, “Inuka, Balaki na usikilize. Nisikilize mimi wewe mwana wa Zippori.

19Mungu siyo mtu, kwamba umdanganye, au mwanadamu awezaye kubadili mawazo. Je, alishawahi kuahidi kitu pasipo kukitekeleza? Je, alishawahi kusema kuwa atafanya kitu bila kufanya kama alivyosema?
20Tazama, Mimi nimeamriwa kuwabariki. Mungu ametoa baraka, nami siwezi kuibadilisha.
21Hajawahi kuona magumu katika Yakobo au tabu katika Israeli. BWANA Mungu wao yuko pamoja nao, na kelele za wafalme wao ziko pamoja nao.
22Mungu aliwatoa Misri kwa nguvu kama za nyati.
23Hakuna uganga utakaofanikiwa dhidi ya Yakobo, na hakuna uchawi utakaomwumiza Israeli. Badala yake, itasemwa juu ya Yakobo na Israeli, 'Tazama kile ambacho Mungu amefanya!'
24Tazama, watu wanainuka kama simba jike, kama vile simba ainukavyo na kuvamia. Halali chini mpaka ale windo lake na kunywa damu ya windo lake,”
25Kisha Balaki akamwambia Balaamu, “Kamwe usiwalaani wala kuwabariki.”
26Lakini Balaamu akamjibu Balaki, “Sijakuambia kuwa nitasema yote ambayo BWANA ananiambia kusema?
27Balaki akamwambia Balaamu, “Njoo sasa, Nami nitakupeleka mahali pengine. Labda kule itampendeza Mungu kunilaania hawa hawa watu.”
28Kwa hiyo Balaki akampeleka Balaamu juu ya Mlima Peori, ambao unalitazama chini lile jangwa,
29Balaamu akamwambia Balaki, “Nijengee madhabahu saba hapa na uniandalie mafahari saba na kondoo duume saba.
30“Kwa hiyo Balaki akafanya kama alivyoambiwa; akatoa sadaka ya fahari na kondoo mume kwenye kila madhabahu.