Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu

Hesabu 31

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1BWANA alinena na Musa na kumwambia,
2“Uwalipizie kisasi Wamidiani kwa kile walichowafanya Waisraeli. Baada ya kufanya hivyo utakufa na kukusanyika na watu wako.”
3Kwa hiyo Musa akawaambia watu. Akasema, “andaeni baadhi ya majeshi yenu kwa ajili ya vita ili kwamba wakawapige Wamidiani na kubeba kiapo cha BWANA.
4Kwa kila kabila la Israeli watatuma askari elfu moja kwa ajili ya vita.”
5Kwa hiyo kati ya wanaume maelfu elfu wa Israeli, wanaume elfu moja walitolewa kwa ajili ya vita, jumla ya wanaume elfu kumi na mbili.
6Kisha Musa akawatuma kwenda vitani, elfu moja toka kila kabila pamoja na Finehasi mwana wa Eliazari kuhanai, wakiwa na vitu kutoka mahali patakatifu wakiwa na matarumbeta kwa ajili ya ishara za sauti.
7Wakapigana na Midiani, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa. Wakamwua kila mwanaume.
8Wakawaua wafalme wa Midiani pamoja na wengine waliowaua ni: Evi, Rekimu, Zuri, Huri, na Reba, hawa walaikuwa ndio waflme watano wa Midiani. pia walimwua Balaamu mwana wa Beori, kwa upanga.
9Jeshi la Israeli likawachukua mateka wanawake wa Midiani, watoto wao, mifugo yao yote, kondoo wao na bidhaa zao zote. walivichukua hivi kama mateka.
10Waliichoma moto miji yao yote walimoishi na kambi zao zote.
11Walichukua vitu vyote na wafungwa, watu na wanyama.
12Wakawaleta mateka, nyara, na wakakamata vitu wakavileta kwa Musa, na Eliazari kuhani, na kwa jamii ya watu wa Israeli. Wakavileta hivi vitu kambini katika uwanda wa Moabu, kule Yorodani karibu na Yeriko.
13Musa, Eliazari kuhani, pamoja na viongozi wa watu wakaenda kukutana nao nje ya kambi.
14Lakini Musa alikuwa na hasira dhidi ya viongozi wa jeshi, Wale majemedari wa maelfu na maakida wa mamia, waliotoka kupigana.
15Musa akawaambia, “Je, mmeawaacha wanawake wote kuishi?
16Tazama, wanawake hawa ndio waliosababisha watu wa Israeli, kwa kupitia ushauri wa Balaamu, kufanya dhambi dhidi ya BWANA huko Peori, wakati ile tauni iliposambaa kwa watu wa Mungu.
17Sasa basi, ueni kila mwanaume kuanzia wadogo, na ueni kila mwanamke aliyelala na mwanamume.
18Lakini chukueni wale mabinti wadogo ambao hawajalala na mwanamume.
19Mtaweka kambi nje na kambi za Israeli kwa muda wa siku saba. Ninyi wote ambao mmeua watu au ambao mmegusa maiti yeyote mtajitakasa wenyewe katika siku ya tatu na katika siku ya saba - ninyi na mateka wenu.
20Na mtayatakasa mavazi yenu yote, na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi za wanyama, na manyoya ya mbuzi, na kila kitu kilichotengenezwa kwa mbao.”
21Eliazarai kuahani akawaambia wale wanajeshi waliokuwa wameenda vitani, “Hii ni amri ya sheria ambayo BWANA alimpa Musa:
22Zile dhahabu, fedha, vyuma, bati, risasi,
23na kila kitu knaweza kuhhimili moto, mtakiweka katka moto, navyo vitakuwa safi. Nakisha mtavitakasa vitu hivyo na maji ya farakano. Na vitu vyote ambavyo haviwezi kupita katika moto, mtavitakasa kwa maji hayo.
24Na mtazifua nguao zenu katika siku ya saba, ndipo mtakapokuwa safi. Baada ya hapo mnaweza kurudi kwenye kambi za Israeli.”
25Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,
26“Vihesabu vitu vyote vilivyochukuliwa nyara, wote watu na wanyama. Wewe, Eliazari kuhani, na viongozi wa watu kufuata koo
27watavigawa hivi vitu katika mkundi mawili. Mvigawe kwa wanajeshi walioenda kupigana na kwa watu wote.
28Kisha toza kodi ambayo itatolewa kwangu kutoka kwa wanajeshi waliokuwa wameenda vitani. Hii kodi itakuwa moja kati ya mia tano, katika watu, ng'ombe, punda, kondoo, au mbuzi.
29Uichukue hii kodi kutoka katika nusu yao na umpe Eliazari kuhani kwa ajili ya sadaka itakayotolewa kwangu.
30Pia kutoka katika nusu ya watu wa Israeli, utachukua moja kati ya hamsini -kutoka vitu, ng'ombe, punda, na mbuzi. Uvitoe hivi kwa Walawi wanaotumika katika masikani yangu.”
31Kwa hiyo Musa na Eliazari kuhani wakafanya kama BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa.
32Sasa zile nyara zilizokuwa zimebaki ambazo wanajeshi walikuwa wameteka zilikuwa kondoo 675, 000,
33maksai elfu sabini na mbili,
34punda elfu sitini na moja,
35na wanawake elfu thelathini na mbili ambao walikuwa hawajalala na mwanamume yeyote.
36Ile hesabu ya nusu iliyokuwa imetunzwa kwa ajili ya wanajeshi ilikuwa kondoo 337, 000. Ile sehemu ya
37BWANA ya kondoo ilikuwa kondoo 675.
38Maksai walikuwa elfu thelathini na sita ambayo kodi ya BWANA ilikuwa sabini na mbili.
39Punda walikuwa 30, 500 ambao sehemu ya BWANA ilikuwa sitini na moja.
40Watu walikuwa wanawake elfu kumi na sita ambao kodi ya BWANA ilikuwa thelathini na mbili.
41Musa aliichukua ile kodi ambayo ilitakiwa kuwekwa sadaka kwa BWANA. Akampatia Eliazari kuhani, kama BWANA alivyomwamuru Musa.
42Ile nusu ya watu wa Israeli ambayo Musa alikuwa ameichukua toka kwa wanawjeshi waliokuwa wameenda vitani -
43ile nusu y a watu ilikuwa kondoo 337, 500,
44maksai elfu thelathini na sita,
45punda 30, 500,
46na wanawake elfu kumi na sita.
47Kutoka kwenye nusu ya watu wa Israeli, Musa alichukua moja katika hamsini, wote watu na wanyama. Aliwapa Walawi ambao huitumikia masikani ya BWANA, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.
48Kisha wale maakida wa jeshi, makamanda wa elfu na makapteni wa mamia, wakaja kwa Musa.
49Wakamwambia, “watumishi wako wamewahesabu wanajeshi ambao wako chini yetu, hakuna hata mmoja wao aliyekosa.
50Tumemletea BWANA sadaka, ambayo kila mmoja amepata, vitu vya dhahabu, metali, timbi, pete za mhuri, vipini na vikuku, ili kujifanyia upatanisho kwa BWANA.”
51Musa na Eliazari kuhani akapokea kutoka kwao dhahabu na vitu vyote vilivyotengenezwa kwa ufundi.
52Vitu vyote vya sadaka ya dhahabu ambavyo walimpa BWANA- sadaka toka kwa makamanda wa maelfu na kutoka kwa makepteni wa mamia - vilikuwa na uzito wa shekeli 16, 750.
53Kila mwanajeshi alikuwa ameteka nyara ya kila mtu kwa ajili yake.
54Musa na Eliazari kuhani wakazichukuazile dhahabu toka kwa makamanda wa maelfu na makepteni wa mamia. Wakavipeleka kwenye hema ya kukutania kama ukumbusho wa watu wa Israeli kwa BWANA.