1Ilitokea baada ya tauni ambayo BWANA alimwambia Musa na Eliazari mwana wa Haruni kuhani, Alisema,
2Wahesabu watu wote wa Israeli, kuanzia miaka ishirini na zaidi, kwa jamaa ya familia zao wote ambao wanaweza kwenda kwenye vita kwa ajili ya Israeli.”
3Kwa hiyo Musa na Eliazari kuhani wakawaambia katika uwanda wa Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko na kusema,
4Wahesabuni watu, kuanzi umri wa miaka ishirini na zaidi kama BWANA alivyomwamuru Musa na watu wa Israeli walitoka katika nchi ya Misri.”
5Reubeni ndiye aliyekuwa wa kwanza, Kutoka kwa mwana wake Hanoki ulitokea ukoo wa Wahanoki. Kutoka kwa Palu ulitokea ukoo wa Wapalu.
6Kutoka Hezroni. ulitokea ukoo wa Wahezroni. Kutoka kwa Kami ulitokea ukoo wa Wakami.
7Hizi ndizo zilikuwa koo za uzao wa Reubeni, ambzo idadi yao ilikuwa wanaume 43, 730.
8Eliabu alikuwa mwana wa Palu.
9Wana wa Eliabu walikuwa ni Nemueli, Dathani. na Abiramu. Hawa ni walewale Dathani na Abiramu waliomfuata Kora waliompinga Musa na Haruni na kumpinga BWANA.
10Pale ambapo dunia ilifungua kinywa na kuwameza pamoja na Kora wakati ambapo wafuasi wa Kora walikufa. Wakati ule, moto uliteketeza wanaume 250, amboa wlikuwa ishara ya onyo.
11Lakini uzao wa Kora haukufa.
12Ukoo wa uzao wa Simeoni walikuwa hawa wafuatao: Kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli, kwa Jamini, ukoo wa Wajamini, kwa Jakini, ukoo wa Wajakini,
13kwa Zera, ukoo wa Wazera, kwa Shauli, ukoo wa Washauli.
14Hizi ndizo koo za uzao wa Simeoni, idadi yao ilikuwa wanaume 22, 200.
15Koo za uzao wa Gadi zilikuwa hizi: Kwa Zefoni, Ukoo wa Wazefoni, kwa Hagi, ukoo wa Wahagi, kwa Shuni, ukoo wa Washuni,
16kwa Ozini, ukoo wa Waozini, kwa Eri, ukoo wa Waeri,
17kwa Arodi, ukoo wa Waarodi, kwa Areli, ukoo wa Waareli.
18Hizi ndizo koo za uzao wa Gadi, idadi yao walikuwa wanaume 40, 500.
19Wana wa Yuda walikwa Er na Onani, lakini hawa walifia katika nchi ya Kanaani.
20Koo zingine za uzao wa Yuda zilikuwa hizi: Kwa Shela, ukoo wa Washela, kwa Perezi, ukoo wa Waperezi, na kwa Zera, ukoo wa Wazera.
21Uzao wa Perezi walikuwa hawa: Kwa Hezroni, ukoo wa Wahezroni, kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.
22Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda, idadi yao ilikuwa wanaume 76, 500.
23Koo za uzao wa Isakari zilikuwa hizi: Kwa Tola, ukoo wa Watola, kwa Puva, ukoo wa Wapuva,
24kwa Jashubu, ukoo wa Wajashubu, kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.
25Hizi ndizo zilikuwa koo za Isakari, Idadi yao ilikuwa wanaume 64, 300.
26Koo za uzao wa Zabuloni zilikuwa hizi: Kwa Seredi, ukoo wa Waseredi, kwa Eloni, ukoo wa Waeloni, kwa Jahaleeli, ukoo wa Wajahaleeli.
27Hizi ndizo zilikuwa koo za Zabuloni, idadi y ao ilikuwa wanaume 60, 500.
28Koo za uzao wa Ysufu zilikuwa Manase na Efraimu.
29Huu ndio uliokuwa uzao wa Manase: Kwa Machiri, ukoo wa Wamachiri (Machiri ndiye aliyekuwa baba wa Giliedi), kwa Giliedi, ukoo wa Wagiliedi.
30Wazo wa Giliedi walikuwa hawa wfuatao: Kwa Lezeri, ukoo wa Walezeri, kwa Helweki, ukoo wa Waheleki, kwa Asrieli,
31ukoo wa Asrieli wa Waasrieli, kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu,
32kwa Shemida, ukoo wa Washemida, kwa Hefa, ukoo wa Wahefa.
33Zelofehadi mwana wa Hefa hakuwa na watoto wa kiume bali alikuwa na mabinti. Majina ya binti zake yalikuwa Mahilahi, Noha, Hoglaha, Milika, na Tiriza.
34Hizi ndizo koo za Manase, idadi yao ilikuwa wanaume 52, 700.
35Koo za wana wa uzao wa Efraimu zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Shuthelaha, ukoo wa Washutheleha, kwa Becheri, ukoo wa Wabecheri, kwa Tahana, ukoo wa Watahana.
36Uzao wa Shuthelaha walikuwa, kwa Erani, ukoo wa Waerani.
37Hizi ndizo koo za uzao wa Efraimu, idadi yao ilikuwa wanaume 32, 500. Huu ndio uzao wa Yusufu, uliohesabiwa toka kila koo zao.
38Koo za uzao wa Benjamini zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Bela ukoo wa Wabela, kwa Ashibeli, ukoo wa Washibeli, kwa Ahiramu, ukoo wa Wahiramu,
39kwa Shefufamu, ukoo wa Washefumamu, kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.
40Wana wa Bela walikuwa ni Ardi na Naamani. Kutoka kwa Ardi ulijitokeza ukoo wa Waardi, na kutoka kwa Naamani ukajaitokeza ukoo wa Wanaamani.
41Hizi ndizo koo za uzao wa Benjamini. Idadai yao ilikuwa wanaume 45, 600.
42Kooo za uzao wa Dani zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizi ndizo koo za uzao wa Dani.
43Idadi ya koo zote za Washuhamu ilikuwa wanaume 64, 400.
44Koo za uzao wa Asheri zilikuwa zifuatazo: Kwa Imna, ukoo wa Waimna, kwa Ishvi, ukoo wa Waishivi, kwa Beria, ukoo wa Waberia.
45Uzao wa Beria walikuwa hawa: Kwa Heberi, ukoo wa Waheberi, kwa Malikieli, ukoo wa Wamalikieli.
46Jina la binti wa Asheri lilikuwa Sera.
47Hizi ndizo koo za uzao wa Asheri, idadi yao ilikuwa wanaume 53, 400.
48Koo za uzao wa Naftali zilikuwa zifuatazo: Kwa Jahazeeli, ukoo wa Wajahazeel, kwa Guni, ukoo wa Waguni,
49kwa Jezeri, ukoo wa Wajezeri, kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.
50Hizi ndizo zilizokuwa koo za uzao wa Naftali, idadi yao walikuwa wanaume 45, 000.
51Hii ndiyo iliyokuwa jumla kuu ya wanaume wa Israeli: 601, 730.
52BWANA akanena na Musa akamwambia,
53Ile ardhi itagawanywa kati ya wanaume hawa kama urithi wao kwa kufuata idadi ya majina yao.
54Kwa zile koo kubwa utawagawia urithi mkubwa, na kwa koo ndogo ndogo utawagawia urithi kidogo. Kwa kila familia utawapa urithi kufuata idadi ya wanaume waliohesabiwa.
55Lakini ardhi itagawiwa kwa kupigiwa kura. Watairithi nchi kama itakavyogawiwa kwa kufuata koo za mababu.
56Urithi huu utagiwiwa kufuata koo kubwa na ndogo, watagawiwa kwa kufuata kura zitakavyokuwa.
57Koo za Walawi, zilizohesabiwa kwa kufuata ukoo kwa ukoo, walikuwa hivi: Kwa Gerishoni, ukoo wa Wagerishoni, kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi, kwa Merari, ukoo wa Wamerari.
58Koo za walawi zilikuwa hzi: ukoo wa Walibni, Ukoo wa Wahebroni, ukoo wa Wamahali, ukoo wa Wamushi, na ukoo wa Wakora. Kohathi alikuwa wa uzao wa Amramu.
59Jina la mke wa Amramu lilikuwa Jokibed, wa ukoo wa Lawi, aliyekuwa amezaliwa kwa Walawi kule Misri. Alimzalia Amramu watoto wao, ambao walikuwa ni Haruni, Musa, na Miriamu dada yao.
60Kwa Haruni alizaliwa Nadabu na Abihu, Eliazari na Ithamari.
61Nadabu na Abihu walikufa walipotoa sadaka kwa BWANA sadaka ya moto isiyokubalika.
62Waume walioheabaiwa miionigoni mwao walikuwa elfu ishirini na tatu, hawa nia wale wa umri wa mwezi mmoja na zaidi. Lakini hawakuhesabiwa kati ya wazawa wa Israeli kwa sababu hawakupewa urithi miongoni mwa wana wa Israeli.
63Hawa nadio wale walihesabiwa na Musa na Eliazari kuhani. Waliwahesabu watu wa Israeli katika uwanda wa Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko.
64Lakini miongoni mwa hawa hapakuwa na mwanamume aliyehasabiwa na Musa na Haruni kuhani wakati wana wa uzao wa Israeli walipohesabiwa katika jangwa la Sinai.
65Kwa BWANA alikuwa amesema kuwa kwa hakika watu hao wote wangefia jangwani. Hapakuwa na mtu aliyebaki miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Joshua mwana wa Nuni.