Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu

Hesabu 24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Balaamu alipooa kuwa ilimpendeza BWANA kubariki Israeli, hakwenda, kama hapo awali, kwa kutumia uganga, badala yake akatazama jangwani.
2Akayainua macho yake na kumwona Isreli akiwa kwenye kambi, kila mmoja kwa kabila yake, na Roho wa Mungu akamjia.
3Akapokea huu unabii na kusema, “Balaamu mwana wa Beori anataka kusema, yeye ambaye macho yake yemefunuliwa sana.
4Huongea na kusikia maneno ya Mungu. Huona maono toka kwa Mwenyezi, ambaye mbele zake humwinamia na macho yake yakiwa yamefumbuliwa.
5Jinsi zilivyo nzuri hema zako, ewe Yakobo, mahali unapoishi, Israeli!
6Wamesambaa kama bonde, kama bustani zilizo pembezoni mwa mto, Kama miti ya mishubiri iliyopandwa na BWANA, ni kama mfano wa mielezi pembezoni mwa maji.
7Maji yanatiririka katika ndoo zao, na mbegu zao zimemwagiwa maji vizuri. Mfalme wao atakuwa juu ya Agagi, na ufalme wao utaheshimiwa.
8Mungu anamtoa Misri, na nguvu kama za nyati. Atawameza mataifa wanaopigana nao. Ataivunja mifupa yao katika vipande vipande. atawapiga kwa mishale yake.
9Ananyatia kama simba mume, na kamaa simba jike. Ni nani atakayejaribu kumsumbua? Kila mmoja anayembariki na abarikiwe; na kila mmoja anayemlaani na alaaniwe.”
10Hasira za Balaki zikawaka dhidi ya Balaamu naye akaipiga mikono yake kwa pamoja. Balaki akamwambia Balaamu, “Nilkuita ili uwalaani maadui zangu, Lakini tazama, umewabariki mara tatu.
11Kwa hiyo ondoka uende nyumbani uniache sasa hivi. Nilisema ningekupa zawadi kubwa sana, lakini BWANA amekuzuilia kupata zawadi.”
12Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, “Niliwaambia wale wajumbe ulionitumia,
13'Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitafanya zaidi ya maneno ya BWANA kwa lolote zuri au baya, au kwa chochote ambacho ningetaka kufanya. Ninaweza kusema kile tu ambacho BWANA ananiambia kusema,' Je, sikuwaambia haya?
14Kwa hiyo sasa, tazama, nitarudi kwa watu wangu. Lakini kwanza nikuonye kile ambacho hawa watu watawafanyia watu wako katika siku zijazo.”
15Balaamu alianza unabii huu. Akisema, “Balaamu mwana wa Beori anasema, Mtu yule aliyefumbuliwa macho yake.
16Huu ni unabii wa mtu alisikiaye neno la Mungu, aliye na maarifa toka kwake Yeye aliye juu, aliye na maono kutoka kwa Mwenyezi, Yeye ambaye humpigia magoti macho yakiwa yamefumbuliwa.
17Ninamwona, lakini hayuko hapa sasa. Ninamtazama, lakini siyo karibu. Nyota itatokea katika Yakobo, na fimbp ya enzi itatokea katika Israeli. Naye atawapigapiga viongozi wa Moabu na kuwaharibu wa uzao wa Sethi
18Ndipo Edomu atakapokuwa miliki ya Israeli, na Seiri pia itakuwa milki yao, maadui wa Israeli, ambao Israeli atawashinda kwa nguvu zake.

19Kutoka kwa Yakobo atatoka mfalme ambaye utawala wake naye atawaangamiza waliosalia katika mji.”
20Kisha Balaamu akamtazama Amaleki na akaanza kutoa unabii wake. Alisema, “Amaleki alikuwa mkuu katika mataifa, lakini mwisho wake utakuwa uharibifu.”
21Kisha Balaamu akawatazama Wakeni na akaanza kutoa unabii wake. Akasema, “Mahali unapoishi pana usalama, na viiota vyake viko kwenye miamba.
22Lakini pamoja na hayo, Kaini ataharibiwa na Ashuru atakapowachukua mateka.”
23Kisha Balaamu akanza unabii wake wa mwisho. Akasema, “Ole wake atakayesalia Mungu atakapoyafanya haya?
24Merikebu zitakuja toka pwani ya Kittimu; Zitaivamia Ashuru na kuiharibu Eberi, lakini wao pia wataishia kwenye uharibifu.”
25Kisha Balaamu akainuka na kuondoka. Akarudi nyumbani kwake, na Balaki naye akaondoka.