Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu

Hesabu 28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1BWANA akanena na Musa akamwambia,
2“Waamuru wana wa Isrseli uwaambie, 'Mtanitolea sadaka kwa wakati uliopangwa, chakula cha sadaka yangu kilichotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa ajili yangu.
3Pia uwaambie, 'Hii ni sadaka iliyotengenezwa kwa moto ambayo mtaitoa kwa BWANA- mwanakondoo dume wa mwaka mmoja asiyekuwa na waa, wawili kila siku kuwa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku.
4Mwanakodoo mmoja atatolewa sadaka asubuhi, na mwingine atatolewa sadaka jioni.
5Mtatoa sadaka ya sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta yaliyokamuliwa.
6Hii ni sadaka ya ya kuteketezwa ya kila siku iliyoamriwa mlima Sinai ili kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajili ya BWANA.
7Pamoja na robo ya hini ya sadaka ya kinywaji kwa mmoja wa hao wanakondoo. Utaimimina mahali patakatifu hiyo sadaka ya kinywaji kwa BWANA.
8Yule mwanakondoo mwingine utamtoa sadaka jioni pamoja na sadaka ya unga kama kama yule wa asubuhi alivyotolewa. Pia utatoa tena sadaka ya kinywaji pamoja naye, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA.
9Katika siku ya Sabato utatoa wanakondoo dume wawili, wa umri wa mwaka mmoja kila mmoja wasiokuwa na dosari, na sehemu ya kumi mbili ya efa ya unga mwembamba kwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka ya kinywaji.
10Hii itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa kila siku ya Sabato, kama nyongeza ya ile sadaka ya kila siku pamoja na ile sadaka ya kinywaji.
11Kila mwanzo wa mwezi, mtatoa sadaka za kuteketezwa kwa BWANA. Utatoa sadaka ya fahari wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na wanakondoo dume saba wa umri wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari.
12Pia mtatoa sehemu ya kumi tatu ya efa unga mwembamba kuwa sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta kwa kila fahari, na sehemu za kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta kwa yule kondoo mume mmoja.
13Pia mtatoa sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwanakondoo. Hii itakuwa sadaka ya kuteketezwa, ya kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajilI ya BWANA.
14Sadaka ya kinywaji ya watu itakuwa nusu ya hini ya divai ya yule fahari, sehemu ya tatu ya hini ya kondoo dume, na robo ya hini ya mwanakondoo. Hii ndiyo itakuwa sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi kwa miezi yote ya mwaka.
15Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA. Hii itakuwa nyongeza kwa ile sadaka ya kila siku pamoja na ile sadaka ya viinywaji.
16Katika siku kumi na nne, ya mwezi wa kwanza itakuwa Pasaka ya BWANA.
17Katika sku ya kumi na tano ya mwezi huu kutakuwa na sikukuu. Mtakuka mikate isiyo na chachu kwa siku saba.
18Katika siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu la kumheshimu BWANA. Katika siku hiyo msifanye kazi zenu za kila siku

19Hata hivyo, mtatoa sadaka iliyotengenezwa kwa moto, sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. Mtatoa sadaka ya fahari wawili, kondoo dume mmoja, na kondoo dume saba wa umri wa mwaka mmoja wakamilifu.
20Pamoja na yule fahari, mtatoa sadaka sehemu za tatu efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, pamoja na yule kondoo mume sehemu za pili za kumi.
21Kwa kila wale wanakondoo saba, mtatoa sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta,
22na beberu mmoja kuwa sdaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
23Mtotoa hivi vitu kama sadaka ya nyongeza katika ile sadaka ya kila siku inayotakiwa kila asubuhi.
24Kama ilivyofafanuliwa hapa, mtatoa sadaka hizi kila siku, kwa zile siku saba za Pasaka, kile chakula cha sadaka kilichotengenezwa kwa moto kuwa harufu nzuri kwa BWANA. Hiki kitatolewa kuwa sadaka ya nyongeza ya ile sadaka ya kuteketezwa na pamoja na ile sadaka ya vinywaji.
25Siku ya saba mtakuwa na kusanyiko takatifu ili kumheshimu BWANA, na katika siku hiyo msifanye zile kazi zenu zakila siku.
26Pia katika siku ya malimbuko, mtakapokuwa mnatoa sadaka ya unga mpya katika sikukuu zenu za Majuma, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumheshimu BWANA, na katika siku hiyo msifanye kazi zenu za kila siku.
27Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari wawili wachanga, kondoo mume mmoja, na wanakondoo saba waume wa mwaka mmoja.
28Pamoja na hiyo mtatoa sadaka ya unga: unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa kila fahari na sehemu kumi mbili za yule kondoo mume.
29Toeni sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa kila wale wanakondoo saba,
30na beberu mmoja ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
31Mtakapotoa hao wanyama wasio na dosari, pamoja na sadaka zake za vinywaji, hii itakuwa sadaka ya nyongeza katika zile sadaka za kila siku na pamoja na zile sadaka za unga.'”