Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu

Hesabu 13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, “tuma watu waende kuipeleleza nchi ya Kanani, ambayo nimewapa wana wa Israeli.
2Tuma mwanamume mmoja kutoka kila jamaa ya kabila. Kila mwanamume awe kiongozi katika kabila lake.”
3Musa akawatuma kutoka jangwa la Parani, ili watii amri ya BWANA. Watu wote hao walikuwa viongozi wa watu wa Israeli.
4Majina yao yalikuwa haya yafuatayo: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;
5Kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;
6Kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;
7Kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yusufu,
8Kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;
9Kutoka kabila la Benjamini, Paliti mwana wa Rafu;
10kutoka kabila ya Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi;
11kutoka kabila la Yusufu (hiyo inamaanisha kutoka kabila la Manase), Gadi mwana wa Susi;
12kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemalili;
13kutoka kabila Asheri, Setu mwana wa Mikaili;
14kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Vofisi;
15kutoka kabila la Gadi, Geuli mwana wa Machi.
16Haya ndiyo majina ya wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuipelelza ile nchi. Musa akamwita Hoshea mwana wa Nuni kwa jina la Joshua.
17Musa akawatuma kwenda kuipeleleza ile nchi ya Kanani. Naye akawaambia, “Mkaanzie Negebu hadi mahali pa milima.
18Kaipelelezeni nchi kujua ni nchi ya namna gani. Wachunguzeni watu wake, kama ni watu wenye nguvu au dhaifu, kama ni wachache au ni wengi.

19Chunguzeni nchi hiyo wanayoishi ni nchi ya namna gani. Ni nzuri au mbaya? Miji yao ikoje? Je iko kama kambi au ni miji yenye ngome?
20Chunguzeni ni nchi ya namna gani, kama ni njema kwa mazao au la kama kuna miti au hapana. Mwe hodari mkalete sampuli za mazao ya nchi,” Sasa ni muda wa msimu wa malimbuko ya mizabibu.
21Kwa hiyo wale wanaume wakaenda kuipeleleza ile nchi kutoka jangwa la Sini mpaka Rehobi, karibu na Lebo Hamati.
22Walienda kutoka Negebu nao wakafika Hebroni. Ahimani, Sheshai, na Talmai, Uzao wa Anaki nao walikuweko, Sasa Hebroni ilikuwa imejengwa miaka saba iliyokuwa imepita kabla ya Zoani wa Misri.
23Nao walipofika katika bonde la Eshikoli, walikata matawi ya mizabibu lenye kishada cha zabibu. Na makundi mawili ya wapelelezi wakakibeba kwenye mti. Pia wakaleta makomamanga na mtini.
24Mahali pale paliitwa Eshikoli, kwa sababu ya kishada cha mizabibu ambacho wana wa Israeli walikata kule.
25Baada ya siku arobaini, wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.
26Wakaja kwa Musa, Haruni na kwa watu wote wa Israeli katka jangwa la Parani, kule Kadeshi. Wakaleta taarifa kwao na kwa Waisraeli wote, na kuwaonyesha matunda ya nchi ile.
27Wakamwambia Musa, “Tulifika katika ile nchi uliyotutuma. Kwa hakika ni nchi ya kutiririka maziwa na asali. Na baadhi ya matunda yake ni haya hapa.
28Hata hivyo, watu wanaoishi huko ni wenye nguvu. Miji yao ni mikubwa tena ina maboma. Pia tuliwaona wana wa Anaki huko.
29Waamaleki wanaishi Negebu. Wahiti, Wayebusi, na Waamori nao wanaishi katika milima ya hiyo nchi. Wakanaani wanaishi kando ya bahari na mto Yorodani.”
30Kisha Kalebu akawatuliza watu waliokuwa mbele ya Musa, akasema, “Twendeni tukaiteke nyara hiyo nchi, kwa kuwa tuna uhakika wa kuikamata.”
31Lakini wale watu waliokuwa wameenda naye walisema, “Hatutaweza kuwashinda hao watu kwa kuwa wao ni hodari kuliko sisi.”
32Kwa hiyo wakasambaza taarifa za kukatisha tamaa kwa Wana wa Israeli juu ya nchi ile waliyoipeleleza. Walisema, “Ile nchi tuliyoiona ni nchi inayowala watu wake. Watu wote tuliowaona ni watu warefu.
33Kule tuliiona majitu, wana wa uzao wa Anaki, ambao nii uzao wa majitu. Sisi tulionekana kama panzi machoni mwao tulipojilingsnisha nao, hivyo ndivyo tulivyoonekana machoni mwao pia.”