Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu

Hesabu 27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisah wakaja kwa Musa binti wa Zelofehadi mwana wa Hefa mwana wa Gilied mwana wa Machiri mwana wa Manase, wa ukoo wa Manase mwana wa Yusufu. Hawa ndio waliokuwa binti zake: Mahala, Noha, Hogla, Milika, na Tiriza.
2Walisimama mbele ya Musa, Eliazari kuhani, kwa. viongozi, na mbele ya watu wote langoni mwa hema ya kukutania. Walisema,
3“Baba yetu alifia jangwani. Hakuwa mmoja wa wale waliompinga BWANA katika lile kundi la Kora. Alikufa kwa dhambi zake, na hakuwa na watoto wa kiume.
4Kwa nini jina la baba yetu liondolewe mioingoni mwa ukoo wa jamaa zake kwa sababu ya kukosa wana? Tupeni ardhi miongoni mwa ndugu wa baba zetu.”
5Kwa hiyo Musa alileta shauri hilo mbele za BWANA.
6BWANA akanena na Musa akamwambia, “Binti wa
7Zelofehadi wanasema kitu sahihi. Lazima uwaptie ardhi kama urithi miongoni mwa ndugu wa baba zao, na uhakikishe kuwa urithi wa baba zao wanapata.
8Utawaambia wana wa Israeli na kusema, 'Kama mtu anakufa na hana mtoto wa kiume, basi utaufanya urithi wake wapewe binti zake.
9Kama hana binti, basi urithi wake atapewa kaka zake.
10Kama hana kaka zake basi huo urithi watapewa ndugu wa baba yake.
11Kama baba yake hana ndugu, basi huo urithi atapewa ndugu yake wa karibu katika ukoo, na utauchukua kuwa wake. Hii itakuwa sheria iliyoanzishwa kwa amri kwa ajili ya watu wa Israeli kama BWANA akivyoniamuru.”
12BWANA alimwamia Musa, “Nenda juu ya mlima Abaraimu na uitazama nchi ambyo nimewapa wana wa Israeli.
13Baada ya kuwa umeiona, pia lazima ufe, kama Haruni kaka yako.
14Hii itatokea kwa sababu ulipinga amri yangu katika jangwa la Sini. Pale ambapo maji yalitoka kwenye mwamba, katika hasira yako ulishindwa kuniheshimu mimi kama mtakatifu mbele ya macho ya watu wote.” Haya ni yale maji ya Meriba ya Kadeshi katika jangwa la Sini.
15Ndipo Musa akamwambia BWANA akisema,
16“Wewe, BWANA, Mungu wa wote wenye mwili, uchague mtu awe juu ya watu,
17mtu ambaye atatoka na kuingia kuja kwao na kuwatoa kisha kuwarudisha, ili kwamba watu wako wasije kuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji.”
18BWANA akanena na Musa, “Mchukue Joshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yangu hukaa, na umwekee mikono yako juu yake.

19Umweke mbele ya Eliazari kuhani na mbele ya watu wote, na umwamuru kuwaongoza mbele ya macho yao.
20Utaweka baadhi ya mamlaka yako kwake, ili kwamba watu wote wa Isareli wamtii.
21Ataenda mbele ya Eliazari kuhani ili kutafuta mapenzi yangu kwake kwa ajili ya maamuzi ya kura. Yeye ndiyo atakayetoa amri ili watu kutoka na kuingia, yeye pamoja na watu wa Israeli, ambao ni watu wote.”
22Kwa hiyo Musa akafanya kama alivyoagizwa na BWANA. Alimchukua Joshua na kumweka mbele ya Eliazari kuhani na mbele ya jamii yote.
23Akaweka mikono yake juuy ake na kumwamuru aongoze, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.