Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu

Hesabu 25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Israeli akakaa Shitimu, na wanaume wakaanza kufanya ukahaba na wanawake wa Moabu,
2kwa kuwa Wamoabu waliwakaribishsa kutoa sadaka kwa miungu yao. Kwa hiyo watu wakala na kuisujudia miungu ya Moabu.
3Watu wa Israeli wakaungana kumwabudu Baali wa Peori, na hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya Israeli.
4BWANA akamwambia Musa, “Waue viongozi wote wa watu na uwanyonge mbele yangu ili waonekane wakati wa mchana, ili kwamba hasira yangu kali iondoke kwa Israeli.”
5Kwa hiyo Musa akawaambia viongozi wa Israeli, “Kila mmoja wenu lazima awanyonge watu wake ambao wameshiriki kumwabudu Baali wa Peori.”
6Kisha mtu mmoja wa Israeli akaleta mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa familia yake. Hili lilitokea mbele ya macho ya Musa na watu wa Israeli, wakati walipokuwa wakilia mbele ya lango la hema ya kukutania.
7Finehasi mwana wa Eliazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona hivyo, akainuka kutoka jamii ya watu akachukua mkuki mkononi mwake.
8Akamfuata yule mwanaume Muisraeli hemani na kuwachoma kwa mkuki wote wawili kwenye miili yao, wote yule Muisraeli na yule mwanamke. Kwa hiyo ile tauni ambayo Mungu alikuwa ameituma kwa watu wa Israeli ikakoma.
9Idadi ya wale waliokufa kwa tauni walikuwa elfu ishirini na nne.
10BWANA akanena na Musa, akasema,
11“Finehasi mwana wa Eliazari mwana wa Haruni, kuhani amaigeuza hasira yangu isiwe kwa wana wa Israeli kwa sababu alikuwa na wivu kati yao juu ya wivu wangu. Kwa hiyo sijawaangamiza watu wa Israeli kwa hasira yangu.
12Kwa hiyo waambie, 'BWANA anasema, “Tazama, Ninampa Finehasi agano la amani.
13Kwake na kwa wana wake baada yake, litakuwa agano la kudumu la ukuhani kwa sababu alikuwa na wivu juu yangu, Mungu wake. Amewapatanisha wana wa Israeli.
14Sasa yule Muisraeli aliyeuwawa pamoja na Yule mwanamke Mmidiani alikuwa Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa familia ya uzao wa Simeoni.
15Jina la yule Mmidiani aliyeuwawa lilikuwa Cozibi binti wa Zuri, ambaye alikuwa mkuu wa familia wa kabila huko Midiani.
16Kwa hiyo BWANA akanena na Musa na kusema,
17“Watendee Wamidiani kama maadui na uwaangamize, kwa kuwa waliwatendea kama maadui
18kwa kuwadanganya. Waliwaongoza katika uovu kwa swala la Peori na kwa swala la dada yao Cozibi, binti wa kiongozi wa Wamidiani, ambaye aliuawa siku ile ya tauni kwa swala la Peori.”