4Habili pia, alileta sehemu ya wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona. Yahwe akamkubali Habili pamoja na sadaka yake,
5lakini Kaini pamoja na sadaka yake Mungu hakuikubali. Kwa hiyo Kaini alikasirika sana, na uso wake ukakunjamana.
6Yahwe akamwambia Kaini, “kwa nini umekasirika na kwa nini uso wako umekunjamana?
7Kama ukifanya vema, je hutapata kibali? lakini kama hutafanya lilio jema, dhambi iko inakuotea mlangoni na inatamani kukutawala, lakini inakupasa uishinde.
8Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. (Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, “twende mashambani.” Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua).
9Kisha Yahwe akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Habili yuko wapi?” Akasema, “sijui. Je mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”
10Yahwe akasema, “umefanya nini? damu ya ndugu yako inaniita mimi kutokea ardhini.
11Na sasa umelaaniwa wewe kutoka ardhi ambayo imefungua kinywa chake kupokea damu ya ndugu yako kutoka mikononi mwako.
12Utakapo ilima ardhi, kuanzia sasa na kuendelea haita kuzalia wewe nguvu yake. Utakuwa mkimbizi na mtu asiye na makao duniani.”
13Kaini akamwambia Yahwe, “Adhabu yangu ni kubwa kuliko uwezo wangu wa kustahimili.
14Kwa hakika umenifukuza siku hii ya leo kutoka kwenye ardhi hii, na sitaonekana mbele ya uso wako. Nitakuwa mkimbizi na mtu nisiye na makao katika dunia, na yeyote atakaye niona ataniua.”
15Yahwe akamwambia, “ikiwa mtuyeyote atamuua Kaini, kisasi kitakuwa juu yake mara saba.” Kisha Yahwe akaweka alama juu ya Kaini, ili kwamba kama mtu awayeyote akimuona, mtu huyo asimshambulie.
16Kwa hiyo Kaini akatoka mbele ya uwepo wa Yahwe na akaishi katika nchi ya Nodi, mashariki mwa Edeni.