1Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya wana wa Nuhu, ambao ni, Shemu, Hamu, na Yafethi. Wana wa kiume walizaliwa kwao baada ya gharika.
2Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Masheki, na Tirasi.
3Na wana wa Gomeri walikuwa Ashikenazi, Rifathi na Togama.
4Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Dodanimu.
5Kutoka kwa hawa watu wa pwani waligawanyika na kwenda kwenye ardhi zao, kila mtu na lugha yake, kufuatana na koo zao, kwa mataifa yao.
6Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misraimu, Putu, na Kanaani.
7Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.
8Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikuwa hodari wa kwanza juu ya nchi.
9Alikuwa mwindaji mkuu mbele ya Yahwe. Hii ndiyo sababu hunenwa, “Kama Nimrod mwindaji mkuu mbele za Yahwe.”
10Miji ya kwanza ya ufalme wake ilikuwa Babeli, Ereku, Akadi na Kalne, katika ichi ya Shinari.
11Kutoka katika nchi ile alikwenda Ashuru na akajenga Ninawi, Rehoboth- iri na Kala,
12na Raseni ambao ulikuwa kati ya Ninawi na Kala. Ulikuwa mji mkubwa.
13Misraimu akazaa Waludi, Waanami, Walehabi, na Wanaftuhi,
14Wapathrusi na Wakasluhi (ambao kwao Wafilisti walitokea), na Wakaftori.
15Kanaani akamzaa Sidono, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
16pia na Myebusi, na Mwamori, Mgirgashi,
17Mhivi, Mwarki, Msini,
18Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi. Baadaye koo za wakanaani zikasambaa.
19Mpaka wa Wakanaani ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza, na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha.
20Hawa walikuwa wana wa Ham, kwa koo zao, kwa lugha zao, katika ardhi zao na katika mataifa yao.
21Pia walizaliwa wana kwa Shemu, ndugu yake mkubwa wa Yafethi. Shemu pia alikuwa baba yao na watu wote wa Eberi.
22Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Alfaksadi, Ludi, na Aramu.
23Wana wa Aramu walikuwa ni Usi, Huli, Getheri, na Mashi.
24Arfaksadi akamzaa Sela, na Sela akamzaa Eber.
25Eberi akazaa wana wawili wa kiume. Jina la mmoja aliitwa Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika. Jina la ndugu yake aliitwa Yoktani.
26Yoktani akamzaa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
27Hadoram, Uzali, Dikla,
28Obali, Abimaeli, Sheba,
29Ofiri, Havila, na Yobabi. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
30Mpaka wao ulikuwa unaanzia Mesha, hadi Sefari, mlima wa mashariki.
31Hawa walikuwa wana wa Shemu, kulingana na koo zao na lugha zao, katika ardhi zao kulingana na mataifa yao.
32Hizi zilikuwa koo za wana wa Nuhu, kulingana na vizazi vyao, kwa mataifa yao. Kutokea kwa hawa mataifa yaligawanyika na kwenda juu ya nchi baada ya gharika.