Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mwanzo

Mwanzo 13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa hiyo Abram akaondoka akatoka Misri na akaenda Negebu, Yeye, mke wake, na vyote alivyokuwa navyo. Lutu pia akaenda pamoja naye.
2Na sasa Abram alikuwa tajiri wa mifugo, fedha na dhahabu.
3Aliendelea na safari yake kutoka Negebu hadi Betheli, mahali ambapo hema yake ilikuwa tangu mwanzo, kati ya Betheli na mji wa Ai.
4Akaenda mahali ambapo madhabahu ilikuwa imejengwa mwanzoni. Hapa akaliitia jina la Yahwe.
5aliyekuwa anasafiri na Abram, alikuwa pia na ngo'mbe, makundi ya mifugo, na mahema.
6Nchi haikuwatosha wote kukaa pamoja karibu kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi sana, kiasi kwamba hawakuweza kukaa pamoja.
7Pia, kulikuwa na ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abram na wachunga wanyama wa Lutu. Wakanaani pamoja na Waperizi walikuwa wakiishi katika nchi ile wakati huo.
8Kwa hiyo Abram akamwambia Lutu, “Pasiwe na ugomvi kati yako na mimi, na kati ya wachunga wanyama wako na wachunga wanyama wangu; licha ya hayo sisi ni familia.
9Je nchi hii yote haiko mbele yako? Nenda na ujitenge na mi. Ikiwa utakwenda kushoto, mimi nitakwenda kulia. au ikiwa utakwenda kulia, mimi nitakwenda kushoto.”
10Kwa hiyo Lutu akatazama, na akaona kuwa nchi yote tambarare ya Yorodani ilikuwa na maji kila mahali hadi Zoari, kama vile bustani ya Yahwe, na kama nchi ya Misri. Hii ilikuwa ni kabla Yahwe hajaiangamiza Sodoma na Gomora.
11Kwa hiyo Lutu akajichagulia yeye mwenyewe nchi tambarare ya Yorodani na akasafiri mashariki, na ndugu hawa wakatengana wao kwa wao.
12Abram akaishi katika nchi ya Kanaani, na Lutu akaishi katika miji ya tambarare. Akatandaza hema zake hadi Sodoma.
13Na sasa watu wa Sodoma walikuwa waovu na wenye dhambi nyingi dhidi ya Yahwe.
14Yahwe akamwambia Abram baada ya Lutu kuondoka kwake, “Angalia kuanzia mahali ulipo simama hadi kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi.
15Nchi yote hii uionayo, nitakupatia wewe pamoja na uzao wako milele.
16Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama mavumbi ya nchi, kiasi kwamba kama kuna mtu anaweza kuhesabu mavumbi ya nchi, ndipo na uzao wako pia utahesabika.
17Inuka, tembea katika urefu na upana wa nchi hii, kwa kuwa nitakupatia.”
18Kwa hiyo Abram akachukua hema yake, akaja na kukaa katika mwaloni wa Mamre, ambao uko Hebroni, na pale akajenga Madhabahu ya Yahwe.