Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mwanzo

Mwanzo 22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ikawa kwamba baada ya mambo hayo Mungu akampima Abraham. Akamwambia, “Abraham!” Abraham akasema, “Mimi hapa.”
2Kisha Mungu akasema, “Mchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, na uende katika nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa mahali pale juu ya moja ya milima hiyo, ambayo nitakwambia.”
3Kwa hiyo Abraham akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukuwa vijana wake wawili, pamoja na Isaka mwanawe. Akakata kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akapanga safari kwenda mahali ambapo Mungu alimwambia.
4Siku ya tatu Abraham akatazama juu na akaona mahali pakiwa mbali.
5Abraham akawambia vijana wake, “kaeni hapa pamoja na punda, mimi pamoja na Isaka tutakwenda pale. Tutaabudu na kisha tutarudi hapa penu.”
6Ndipo Abraham akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa akaziweka juu ya Isaka mwanawe. Mkononi mwake akachukua moto na kisu; na wote wawili wakaondoka pamoja.
7Isaka akazungumza na Abraham baba yake akisema, “Baba yangu,” naye akasema, “Ndiyo mwanangu.” Akasema, “Tazama huu ni moto na kuni, lakini yuko wapi mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”
8Abraham akasema, “Mungu mwenyewe atatupatia mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mwanangu.” Kwa hiyo wakaendelea, wote wawili pamoja.
9Walipofika mahali ambapo Mungu alikuwa amemwambia, Abraham akajenga madhabahu pale na akaweka kuni juu yake. Kisha akamfunga Isaka mwanawe, na akamlaza juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.
10Abraham akanyoosha mkono wake akachukua kisu ili kumuua mwanawe.
11Ndipo malaika wa Yahwe akamwita kutoka mbinguni na kusema, “Abraham, Abraham!” naye akasema, “Mimi hapa.”
12Akasema, “usinyooshe mkono wako juu ya kijana, wala usifanye jambo lolote kumdhuru, kwa kuwa sasa najua unamcha Mungu, kwa kuona kuwa hukumzuilia mwanao, mwanao wa pekee, kwa ajili yangu.”
13Abraham akatazama juu na tazama, nyuma yake kulikuwa na kondoo mume amenaswa pembe zake kichakani. Abraham akaenda akamchukua kondoo na akamtoa kama sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
14Kwa hiyo Abraham akapaita mahali pale, Yahwe atatoa,” na panaitwa hivyo hata leo. “Juu ya mlima wa Yahwe itatolewa.”
15Malaika wa Yahwe akamwita Abraham kwa mara ya pili kutoka mbinguni
16na kusema - Hiki ni kiapo cha Yahwe, “Kwa ajili ya nafsi yangu nimeapa kwamba kwa kuwa umefanya jambo hili, na hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
17hakika nitakubariki na nitakuzidishia uzao wako kama nyota za angani, na kama mchanga ulioko kwenye ufukwe wa bahari; na uzao wakowatamiliki lango la adui zao.
18Kupitia uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa, kwa sababu umetii sauti yangu.”

19Kwa hiyo Abraham akarejea kwa vijana wake, na wakaondoka wakaenda pamoja Beerisheba, hivyo akakaa Beerisheba.
20Ikawa kwamba baada ya mambo haya ambayo Abraham aliambiwa, “Milka amemzalia pia watoto, ndugu yako Nahori.”
21Hawa walikuwa ni Usi mzaliwa wa kwanza, Busi ndugu yake, Kemueli aliye mzaa Aramu,
22Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu, na Bethueli.
23Bethuel akamzaa Rebeka. Hawa walikuwa ni wale watoto wanane ambao Milka alizaa kwa Nahori, ndugu yake na Abraham.
24Suria wake, ambaye aliitwa Reuma, pia akamzaa Teba, Gahamu, Tahashi, na Maaka.