Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Marko - Marko 8

Marko 8:1-26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Katika siku hizo, kulikuwa tena na umati mkubwa, na hawakuwa na chakula. Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia,
2“Ninauhurumia umati huu, wameendelea kuwa nami kwa siku tatu na hawana chakula.
3Nikiwatawanya warudi majumbani kwao bila kula wanaweza wakazimia njiani kwa njaa. Na baadhi yao wametoka mbali sana.”
4Wanafunzi wake wakamjibu, “Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwashibisha watu hawa katika eneo hili lililoachwa?”
5Akawauliza, “mna vipande vingapi vya mikate?” Wakasema, “Saba”.
6Aliuamuru umati ukae chini. Akachukua mikate saba, akamshukuru Mungu, na kuivunja. Akawapa wanafunzi wake waiweke mbele yao, nao wakaiweka mbele ya umati.
7Pia walikuwa na samaki wadogo wachache, na baada ya kushukuru, aliwaamuru wanafunzi wake wawagawie hivi pia.
8Walikula na wakatosheka. Na walikusanya vipande vilivyo baki, vikapu vikubwa saba.
9Walikaribia watu elfu nne. Na aliwaacha waende.
10Mara aliingia kwenye mashua na wanafunzi wake, na wakaenda katika ukanda ya Dalmanuta.
11Kisha Mafarisayo walitoka nje na kuanza kubishana naye. Walitaka awape ishara kutoka mbinguni, kwa kumjaribu.
12Akatafakari kwa kina moyoni mwake akasema, “Kwa nini kizazi hiki kinatafuta ishara? Nawaambia ninyi kweli, hakuna ishara itakayotolewa kwa kizazi hiki.”
13Kisha akawaacha, akaingia ndani ya mashua tena, akaondoka kuelekea upande mwingine.
14Wakati huo wanafunzi walisahau kuchukua mikate. Hawakuwa na mikate zaidi ya kipande kimoja kilichokuwa kwenye mashua.
15Aliwaonya na kusema, “Muwe macho na mjilinde dhidi ya chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.
16Wanafunzi wakasemezana wao kwa wao, “Ni kwa sababu hatuna mikate.”
17Yesu alilitambua hili, na akawaambia, “Kwa nini mnasemezana kuhusu kutokuwa na mikate? Hamjajua bado? Hamuelewi? Mioyo yenu imekuwa miepesi?
18Mna macho, hamuoni? Mna masikio, hamsikii? Hamkumbuki?
19Nilipoigawanya mikate mitano kwa watu elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vilivyo jaa vipande vya mikate?” Wakamjibu, “kumi na mbili.”
20“Na nilipoigawanya mikate saba kwa watu elfu nne, mlichukua vikapu vingapi?”
21Wakasema, “Saba.” Akawaambia, “Bado hamuelewi?”
22Wakaja Bethsaida. Watu hao walimleta kwa Yesu mtu kipofu na wakamsihi Yesu amguse.
23Yesu akamshika kwa mkono yule kipofu, na kumwongoza nje ya kijiji. Alipotema mate juu ya macho yake na kunyosha mikono yake juu yake, alimuuliza, “Unaona chochote?”
24Alitazama juu na kusema, “Naona watu wanaonekana kama miti inatembea.”
25Ndipo akanyosha tena mikono yake juu ya macho yake, mtu yule akafungua macho yake, aliona tena, na akaona kila kitu vizuri.
26Yesu alimwacha aende nyumbani na akamwambia, “Usiingie mjini.”

Read Marko 8Marko 8
Compare Marko 8:1-26Marko 8:1-26