Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 19

Luka 19:32-39

Help us?
Click on verse(s) to share them!
32Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia.
33Walipokuwa wanamfungua mwana punda wamiliki wakawaambia, 'Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?'
34Wakasema, `Bwana anamhitaji.'
35Basi, wakampelekea Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana punda na wakampandisha Yesu juu yake.
36Alipokuwa akienda watu wakatandaza mavazi yao barabarani.
37Alipokuwa anateremka mlima wa Mizeituni, jumuiya yote ya wanafunzi wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona,
38wakisema, 'Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana! Amani mbinguni, na utukufu juu!'
39Baadhi ya Mafarisayo katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako.'

Read Luka 19Luka 19
Compare Luka 19:32-39Luka 19:32-39