Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 42

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha Ayubu akamjibu Yahweh na kusema,
2“Ninajua kwamba unaweza kufanya mambo yote, ya kuwa hakuna kusudi lako linaweza kuzuiliwa.
3Ni nani huyo ambaye pasipo maarifa huificha mipango? Kwa kweli nilisema mambo ambayo sikuyaelewa, mambo magumu kwangu kuyafahamu, ambayo juu yake sikujua chochote.
4Uliniambia, 'Sikiliza sasa, nami nitasema; nitakuuliza mambo, nawe utaniambia.'
5Nimekuwa nikikusikia kwa usikivu wa sikio langu, lakini sasa jicho langu linakuona wewe.
6Basi ninajidharau mwenyewe; ninatubu kwa mavumbi na majivu.”
7Ilitokea baada ya kuwa amekwisha kusema maneno hata kwa Ayubu, Yahweh alimwambia Elifazi Mtemani, “Ghadhabu yangu imewaka dhidi yako na dhidi ya marafiki zako wawili kwa kuwa hamkusema maneno ya haki juu yangu kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.
8Sasa basi, jitwalieni mafahari saba na mabeberu saba, kisha mmwendee mtumishi wangu Ayubu na mtoe sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yenu. Ndipo Mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi, nami nitayapokea maombi yake, ili kwamba nisiwashughulikie sawasawa na upumbavu wenu. Maana hamkusema mambo ya haki juu yangu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.”
9Basi Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi na Zofari Mnaamathi walienda na kufanya kama vile Yahweh alivyowaamuru, na Mungu alimtakabali Ayubu.
10Na wakati Ayubu alimpowaombea rafiki zake, Yahweh alirejeza bahati yake. Yahweh alimjalia mara mbili ya kile alichokimiliki hapo awali.
11Ndipo ndugu zake na Ayubu, na wale jamaa zake wote walikuwa wanajuana naye hapo mwanzo, walikuja hapo kwake na kula chakula pamoja naye katika nyumba yake. Waliomboleza pamoja naye na walimfariji kwa ajili majanga yote ambayo Yahweh alikuwa ameyaleta juu yake. Kila mtu alimpa Ayubu kipande cha fedha na pete ya dhahabu.
12Yahweh aliubarikiwa mwisho wa maisha ya Ayubu kuliko mwanzo wake; alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, ngamia elfu sita, jozi elfu moja, na punda jike elfu moja.
13Pia alikuwa na wana saba na mabinti watatu.
14Binti wa kwanza alimwita Yemima, na wa pili Kezia, na wa tatu Kerenihapuki.
15Katika nchi yote hawakupatikana wanawake wazuri kama mabinti wa Ayubu. Baba yao aliwapa urithi miongoni mwa kaka zao.
16Baada ya haya, Ayubu aliishi miaka 140; aliwaona wana wake na wana wa wanawe, hata kizazi cha nne.
17Basi Ayubu alifariki, akiwa mzee na akijawa na siku nyingi.