Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Nyakati

1 Nyakati 8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wana watano wa Benjamini walikuwa Bela mwana wake wa kwanza, Asibeli, Ahara,
2Noha, na Rafa.
3Wana wa Bela walikuwa Adari, Gera, Abihudi,
4Abishau, Naamani, Ahoa,
5Gera, Shefufani, na Huramu.
6Hawa walikuwa uzao wa Ehudi ambao walikuwa vichwa vya koo kwa wakazi wa Geba, ambao walihimizwa kuhamia Manahati:
7Naamani, Ahijahi, na Gera. Wa mwishi, Gera, aliwaongoza katika kuhama. Alikuwa baba wa Uza na Ahihudi.
8Shaharaimu akawa baba wa watoto katika ardhi ya Moabu, baada ya kuwatariki wake zake Hushimu na Baara.
9kwa mke wake Hodeshi, Shaharaimu akawa baba wa Yobabu, Zibia, Mesha, Malkamu,
10Yeuzi, Shachia, na Mirima. Hawa walikuwa wana wake, viongozi katika koo zao.
11Alikwisha kuwa baba wa Abitubi, na Elipaali kwa Hushimu.
12Wana wa Elipaali walikuwa Eba, Mishamu, na Shemedi (ambao walijenga Ono na Lod pamoja na vijiji vilivyozunguka.)
13Pia walikuwako Beria na Shema. Walikuwa vichwa vya koo walizoishi Aijalon, Ambao waliwaondoa wakazi wa Gati.
14Beria alikuwa na wana watatu: Ahio, Shashaki, Jeremothi,
15Zebadia, Aradi, Eda,
16Mikaeli, Ishipa, na Joha.
17Elipaa alikuwa na wana hawa: Zebadia, Meshulamu, Hiziki, Heba, Ishimerai, Izilia, na Yobabu.
19Shimei alikuwa na wana hawa: Yokimu, Zikri, Zabdi,

20Elienai, Zilletai, Elieli,
21Adaia, Beraia, na Shimrati.
22Shashaki alikuwa na wana hawa: Ishipani, Eba, Elieli,
23Abdoni, Zikri, Hanani,
24Hanania, Elamu, Antotoja,
25Ifdeia, na Penueli.
26Yerohamu alikuwa na wana hawa: Shamsherai, Sheharia, Atli,
27Yaareshia, Elija, na Zikri.
28Hawa walikuwa vichwa vya koo na viongozi walioishi Yerusalemu.
29Baba wa Gibeoni, Jeieli, ambaye mke wake aliitwa Maaka, aliishi ndani ya Gibeoni.
30Uzao wake wa kwanza alikuwa Abdoni, akafatia Zuri, Kishi, Baali, Nadab,
31Gedori, Ahio, na Zekari.
32Mwana mwingine wa Yeieli alikuwa Mikloti, ambaye akaja kuwa baba wa Shimea. Pia wanaishi karibu na ndugu zao Yerusalemu.
33Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. Sauli alikuwa baba wa Yonathani, Malkishua, Abinadabu, na Ishbaali.
34Mwana wa Yonathani alikuwa Meribu Baali. Meribu Baali alikuwa baba wa Mika.
35Wana wa Mika walikuwa Pithoni, Meleki, Tarea, and Ahazi.
36Ahazi akawa baba wa Yehoada. Yehoada alikuwa baba wa Amelethi, Azimavethi, na Zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza.
37Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Rafa. Rafa alikuwa baba wa Eleasa. Eleasa alikuwa baba wa Azeli.

38Azeli alikuwa na wana sita: Azrikamu, Bokeru, Ishimaeli, Obadia, na Hanani. Wote hawa walikuwa wana wa Azeli.
39Wana wa Esheki, kaka yake, walikuwa Ulamu mzaliwa wake wa kwanza, Yeushi wa pili, na Elifeleti wa tatu.
40Wana wa Ulamu walikuwa wanaume wa mapambano na warusha mishale wa zuri. Walikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla ya 150. Wote hawa walikuwa uzao wa Benjamini.