Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Maombolezo

Maombolezo 5

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kumbuka, Yahweh, yaliyo tutokea na uone aibu yetu.
2Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni; nyumba zetu kwa wageni.
3Tumekuwa yatima, bila baba, na mama zetu ni kama wajane.
4Lazima tulipe fedha kwa maji tunayo kunywa, na tulipe fedha kupata mbao zetu.
5Hao wanakuja kwetu wamekaribia nyuma yetu; tumechoka na hatuwezi pata mapumziko.
6Tumejitoa kwa Misri na kwa Assiria tupate chakula cha kutosha.
7Baba zetu walifanya dhambi, na hawapo tena, na tumebeba dhambi zao.
8Watumwa walitutawala, na hakuna wa kutuokoa na mikono yao.
9Tunapata mkate wetu pale tunapo hatarisha maisha, kwasababu ya upanga wa nyikani.
10Ngozi zetu zimekuwa na moto kama jiko kwasababu ya joto la njaa.
11Wanawake wanabakwa Sayuni, na mabikra katika mji wa Yuda.
12Watoto wa mfalme wamenyongwa na mikono yao, na hakuna heshima inayoonyeshwa kwa wazee.
13Wanaume vijana wanalizimishwa kusaga mbegu kwa jiwe la kusagia, na wavulana wanajikwa chini ya vifurushi vya kuni.
14Wazee wameacha lango la mji, na vijana wameacha miziki.
15Furaha ya moyo imekoma na kucheza kwetu kumegeuka kilio.
16Taji limeanguka kichwani mwetu; ole wetu, kwa kuwa tumetenda dhambi!
17Kwa kuwa moyo wetu umekuwa unaumwa, na machozi yetu ya fifia, kwa vitu hivi macho yetu yanafifia
18maana Mlima Sayuni umelala ukiwa, mbwa wa mitaani wacheza juu yake.

19Lakini wewe, Yahweh, unatawala milele, na utaketi katika kiti chako cha enzi vizazi na vizazi. Kwanini unatusahau milele?
20Kwanini unatutelekeza kwa siku nyingi?
21Turejeshe kwako, Yahweh, na sisi tutarejea. Fanya upya siku zetu kama zilivyo kuwa hapo zamani -
22vinginevyo labda uwe umetukataa na una hasira kwetu kupita kiasi.