Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Maombolezo

Maombolezo 1

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mji ambao mwanzo ulikuwa na watu wengi sasa umekaa peke yake. Amekuwa kama mjane, japo alikuwa taifa kubwa. Alikuwa mtoto wa mfalme miongoni mwa mataifa, lakini sasa amelazimishwa utumwani.
2Analia na kuomboleza usiku, na machozi yake yanafunika mashavu yake. Hamna ata mpenzi wake anaye mliwaza. Marafiki wake wote wamemsaliti. wamekuwa maadui wake.
3Baada ya umaskini na mateso, Yuda ameenda matekani. Anaishi miongoni mwa mataifa na hapati pumziko lolote. Wanao wakimbiza wamewapata katika upweke wake.
4Barabara za Sayuni zinaomboleza kwasababu hakuna anaye kuja kwenye sherehe iliyo andaliwa. Malango yake yote ni ukiwa. Makuhani wake wote wana sononeka. Mabikra wake wana uzuni na yeye mwenyewe yupo katika ugumu.
5Maadui wake wamekuwa bwana zake; maadui wake wana fanikiwa. Yahweh amemuadhibu kwa dhambi zake nyingi. Watoto wake wadogo wanaenda matekani kwa maadui zake.
6Uzuri umemwacha binti wa Sayuni. Watoto wa mfalme wamekuwa kama ayala ambaye haoni malisho, na wanaenda bila uwezo kwa wanao wakimbiza.
7Katika siku za mateso yake na kutokuwa na nyumba, Yerusalemu itakumbuka hazina zake za dhamani alizo kuwa nazo awali. Wakati watu wake walipo angukia mikononi mwa adui, hakuna aliye msaidia. Maadui waliwaona na kucheka maangamizo yake.
8Yerusalemu ili tenda dhambi sana, hivyo basi, amedhalillika kama kitu kichafu. Wote walio mheshimu sasa wana mdharau kwa kuwa wameona uchi wake. Anasononeka na kujaribu kugeuka pembeni.
9Amekuwa mchafu chini ya sketi yake. Hakuwaza hatima yake. Anguko lake lilikuwa baya. Hakukuwa na wakumliwaza. Alilia, “Angalia mateso yangu, Yahweh, kwa kuwa adui amekuwa mkuu sana.”
10Adui ameeka mkono wake kwenye hazina zetu za dhamani. Ameona mataifa yakiingia sehemu yake takatifu, japo uliamuru wasiingie katika sehemu yako ya kukusanyikia.
11Watu wote wana sononeka wanapo tafuta mkate. Wametoa hazina zao za dhamani kwa ajili ya chakula cha kurejesha uhai wao. Tazama, Yahweh, ni kumbuke mimi, kwa kuwa nimekuwa sina faida.
12Sio kitu kwako, wote mnao pita? Angalia na uone kama kuna mtu mwenye uzuni kama uzuni ninao teswa nao, tangu Yahweh amenitesa mimi katika siku ya hasira yake kali.
13Ni kutoka juu ndipo alipo tuma moto kwenye mifupa yangu na umenishinda. Ametanda nyavu kwa miguu yangu na kunigeuza. Amenifanya ukiwa na dhahifu.
14Nira ya makosa yangu imefungwa na mikono yake. Zimesokotwa na kuekwa shingoni mwangu. Amefanya uweza wangu kushindwa. Bwana amenikabidhi mikononi mwa, na siwezi kusimama.
15Bwana ametupa pembeni wanaume wangu hodari walio niokoa. Ameitisha kusanyiko dhidi yangu kuponda wanaume wangu imara. Bwana amewakanyaga binti bikra wa Yuda kwenye chombo cha kusagia mvinyo.
16Kwa vitu hivi ninalia. Macho yangu, maji yanashuka chini ya macho yangu tangu mfariji aliye paswa kurejesha maisha yangu yuko mbali na mimi. Watoto wangu wamekuwa ukiwa kwasababu adui yangu ameshinda.
17Sayuni ametandaza mikono yake; hakuna wakuwa mliwaza. Yahweh ameamuru hao karibu na Yakobo wawemaadui wake. Yerusalemu ni kitu kichafu kwao.
18Yahweh ni mwenye haki, kwa kuwa nimeasi dhidi ya amri zake. Sikia, ninyi watu, na muone uzuni wangu. Mabikra wangu na wanaume imara wameenda matekani.

19Niliita marafiki zangu, lakini walikuwa na hila kwangu. Makuhani wangu na wazee waliangamia kwenye mji, walipo kuwa wanatafuta chakula cha kurejesha uhai wao.
20Tazama, Yahweh, kwa kuwa nipo kwenye ugumu; tumbo langu lina nguruma, moyo wangu umetibuka ndani yangu, kwa kuwa nimekuwa muasi sana. Nje, upanga umemliza mama, ndani ya nyumba kuna mauti tu.
21Wamesikia sononeko langu, lakini hakuna wakuni liwaza. Maadui zangu wote wamesikia shida zangu na wamefurahi umenifanyia hivi. Umeleta siku uliyo ahidi; sasa acha wawe kama mimi.
22Acha uovu wote uje mbele zako. Shughulika nao kama ulivyo shughulika na mimi kwasababu ya makosa yangu yote. Masononeko yangu ni mengi na moyo umezimia.