Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Maombolezo

Maombolezo 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mimi ni mwanaume nilyeona maangaiko chini ya gongo la hasira ya Yahweh.
2Amenifukuza na kunisababisha kutembea kwenye giza kuliko kwenye nuru.
3Hakika amenigeuzia mkono wake dhidi yangu tena na tena, siku yote.
4Amefanya mwili wangu na ngozi yangu kufifia; amevunja mifupa yangu.
5Amejenga vifusi vya udogo dhidi yangu, na kunizingira na uchungu na ugumu.
6Amefanya ni ishi sehemu za giza, kama hao walio kufa zamani.
7Amejenga ukuta kunizunguka na siwezi kutoroka. Amefanya minyororo yangu mizito
8na japo nina ita na kulilia msaada, anazima maombi yangu.
9Ameziba njia yangu kwa ukuta wa mawe ya kuchonga; amefanya njia yangu mbaya.
10Yeye ni kama dubu anasubiri kunishambulia, simba katika maficho;
11amegeuza pembeni njia zangu, amenifanya ukiwa.
12Amepindisha upinde wake na kunifanya mimi kama lengo la mshale wake.
13Ametoboa maini yangu kwa mishale ya mfuko wake.
14Nilikuwa kichekesho kwa watu wangu wote, kielelezo cha dhihaka yao siku nzima.
15Amenijaza kwa uchungu na kunilazimisha kunywa maji machungu.
16Alivunja meno yangu na kokoto; amenisukuma chini kwenye fumbi.
17Nafsi yangu imenyimwa amani; nimesahau furaha ni nini.
18Hivyo na sema, “Ustahimilivu wangu umeangamia na pia tumaini langu kwa Yahweh.”

19Kumbuka mateso yangu na kuangaika kwangu, maji machungu na uchungu.
20Ninaendelea kukumbuka na nimeinama ndani yangu.
21Lakini ni vuta hili akilini mwangu na hivyo nina matumaini:
22Upendo dhabiti wa Yahweh haukomi na huruma zake haziishi,
23ni mpya kila asubui; uaminifu wako ni mkubwa.
24“Yahweh ni urithi wangu,” Nilisema, hivyo nitamtumainia.
25Yahweh ni mwema kwao wanao msubiri, kwa anaye mtafuta.
26Ni vizuri kusubiri taratibu kwa uwokovu wa Yahweh.
27Ni vizuri kwa mtu kubeba nira katika ujana.
28Acha aketi peke yake katika utulivu, inapo kuwa imewekwa juu yake.
29Acha aeke mdomo wake kwenye vumbi - kunaweza bado kuwa na matumaini.
30Acha atoa shavu lake kwa yeye anaye mpiga, na ajazwe tele kwa aibu.
31Kwa kuwa Bwana hatatukataa milele,
32lakini japo anatia uzuni, ata kuwa na huruma kwa kadiri ya mwingi wa upendo wake dhabiti.
33Kwa kuwa haadhibu kutoka moyoni mwake au kutesa watoto wa mwanadamu.
34Kukanyaga chini ya mguu wafungwa wote wa dunia,
35kumnyima haki mtu mbele ya uwepo wa Aliye Juu,
36mkunyima haki mtu - Bwana hataidhinisha vitu kama hivyo!

37Ni nani aliye zungumza na ikatimia, kama sio Bwana kutamka?
38Sio kutoka mdomoni mwa Aliye Juu majanga na mazuri yanakuja?
39Mtu aliye hai anawezaje kulalamika? Mtu anawezaje kulalamika kwa adhabu ya dhambi zake?
40Natujichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Yahweh.
41Na tunyanyue mioyo yetu na mikono yetu kwa Yahweh mbinguni:
42“Tumekosea na kuasi, na haujasamehe.
43Umejifunika na hasira na kutukimbiza, umeua na haujanusuru.
44Umejifunika na wingu ili kwamba kusiwe na ombi linaloweza kupita.
45Umetufanya kama uchafu na taka miongoni mwa mataifa.
46Maadui wetu wote wametulaani,
47wasiwasi na shimo limetujia, maafa na uharibifu.
48Macho yangu yanatiririka na miferiji ya machozi kwasababu ya watu wangu.
49Macho yangu yatatoa machozi pasipo kikomo; pasipo hauweni,
50mpaka atakapo tazama chini na Yahweh ataona kutoka mbinguni.
51Macho yangu yana ni sababishia uzuni kwasababu ya mabinti wa mji wangu.
52Nimewindwa kama ndege hao walio kuwa maadui zangu; wameniwinda pasipo sababu.
53Wamenitupa kwenye shimo na wakanitupia jiwe,
54na maji yaka mwagika juu ya kichwa changu. Nilisema, “Nimekatwa mbali!”

55Nililiita jna lako, Yahweh, kutoka kina cha shimo.
56Ulisikia sauti yangu. Ulisikia sauti yangu nilipo sema, “Usifunge sikio lako kwa kilio changu cha msaada.”
57Ulikuja karibu siku niliyo kuiita; ulisema, “Usiogope”
58Bwana, ulitetea kesi yangu, uliokoa maisha yangu!
59Yahweh, umeona mabaya waliyo ni fanyia, hukumu kesi yangu.
60Umeona matusi yao, mipango yao yote dhidi yangu -
61Umesikia dhihaka yao, Yahweh, na mipango yao kunihusu.
62Midomo ya hao wanao inuka kinyume changu, na mashtaka yao, inakuja dhidi yangu siku nzima.
63Ngalia jinsi wanavyo keti na kuinuka; wana nidhihaki na nyimbo zao.
64Walipize, Yahweh, kwa kadiri ya waliyo fanya.
65Utaacha mioyo yao bila lawama! Hukumu yako iwe juu yao!
66Una wakimbiza kwa hasira na kuwaharibu nchini ya mbingu, Yahweh!