Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua

Yoshua 5

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mara tu waliposikia wafalme wa Waamori walio upande wa magharibi wa Yordani, na wafalme wote wa Wakanaani waliokuwa katika pwani ya Ziwa kuu, waliposikia ya kwamba Yahweh alikuwa ameyakausha maji ya Yordani mpaka pale waisraeli wote walipomaliza kuvuka, mioyo yao ikayeyuka, na hapakuwa na moyo wowote ndani yao kwa sababu ya watu wa Israeli.
2Kwa wakati huo Yahweh alimwambia Yoshua, “Tengenezeni visu vya mawe na mara moja mwatahiri wanaume wote wa Israeli.”
3Kisha Yoshua alijifanyia visu vya mawe na akawatahiri wanaume wote wa Gibea Haaraloti.
4Na hii ndo sababu ya Yoshua kuwatahiri; wanaume wote waliotoka Misri, pamoja na wanaume wa vita walikuwa wamekwisha kufa njiani katika nyikani, baada ya kukwea kutoka Misri.
5Ingawa wanaume wote waliotoka Misri walikuwa wametahiriwa, bado hapakuwa na kijana yeyote aliyekuwa ametahiriwa kati ya vijana wote waliozaliwa nyikani katika njia ya kutoka Misri.
6Kwasababu watu wa Israeli walitembea nyikani miaka arobaini, mpaka watu wa vita, yaani wanaume wote waliotoka Misri walikufa, kwasababu hawakuitii sauti ya Yahweh. Yahweh aliwaapia kwamba hawataruhusu kuiona nchi ambayo aliwaapia mababa zao kwamba angetupatia sisi, nchi inayotiririka maziwa na asali.
7Na badala yao, Yahweh aliwainua watoto wao kuchukua nafasi zao ambao Yoshua aliwatahiri, kwasababu walikuwa bado hajatahiriwa njiani.
8Walipokwisha kutahiriwa wote, walibaki mahali walipokuwa katika kambi mpaka walipopona.
9Na Yahweh akasema na Yoshua, “Siku hii nimeiondoa kwenu aibu ya Misri.” Hivyo, mahali pale paliitwa Gilgali hadi leo.
10Watu wa Israeli walipiga kambi hapo Gilgali. Waliitunza Pasaka katika siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika uwanda wa Yeriko.
11Na siku iliyofuata baada ya Pasaka, walikula sehemu ya mazao ya nchi, mikate isiyotiwa chachu na nafaka iliyokaangwa katika siku hiyo iyo.
12Mana zilikoma siku ile walipokula mazao ya nchi. Hapakuwa tena na mana kwa watu wa Israeli, bali walikula mazao ya nchi ya Kanaani mwaka huo.
13Wakati Yoshua alipokaribia Yeriko, aliinua macho na kuangalia, na tazama, mtu alikuwa amesimama mbele yake, alikuwa amechomoa upanga wake na ulikuwa mkononi mwake. Yoshua alimwendea na kumwambia, “Je uko kwa ajili yetu au kwa ajli ya maadui zetu?”
14Akajibu, la hasha. Maana mimi ni amiri wa jeshi la Yahweh. Sasa nimekuja. Kisha Yoshua akainamisha uso wake juu ya nchi akaabudu na akamwambia, “Bwana wangu anasema nini kwa mtumwa wake?”
15Amiri wa jeshi la Yahweh akamwambia Musa, “Vua viatu vyako miguuni mwako, kwasababu sehemu uliyosimama ni takatifu.” Na Yoshua akafanya hivyo.