1Kisha wakuu wa koo za Walawi walimwendea Eliazari kuhani, na kwa Yoshua mwana wa Nuni, na kwa viongozi wa familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli.
2Waliwaambia, “Yahweh aliwaagizeni ninyi kwa mkono wa Musa kwamba mtupatieni miji ya kuishi yenye maeneo kwa ajili ya kuchungia ya mifugo.” waliyasema haya huko Shilo katika nchi ya Kanaani.
3Hivyo, kwa agizo la Yahweh, watu wa Israeli waliwapa Walawi kutoka katika urithi wa wao miji ifuatayo pamoja na maeneo yao ya kuchungia.
4Upigaji wa kura kwa ajili ya koo za Wakohathi ulileta matokeo haya: makuhani ambao ni wazawa wa Haruni ambao walitokana na Walawi, walipokea miji kumi na mitatu waliopewa kutoka kwa kabila la Yuda, kutoka kabila la Simoni, na kutoka kabila la Benyamini.
5Koo zilizobaki za Wakohathi walipokea kwa kupiga kura kwa miji kumi kutoka katika kabila za Efraimu, Dani, na kutoka kwa nusu ya kabila la Manase.
6Na watu wazawa wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kwa kupigiwa kura kutoka kwa koo za kabila la Isakari, Asheri, Nafutali, na nusu ya kabila la Manase katika Bashani.
7Watu waliokuwa wazawa wa Merari walipokea miji kumi na miwili kutoka katika makabila ya Rubeni, Gadi na Zabuloni.
8Basi, watu wa Israeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yao ya kuchungia, kwa kupiga kura, kama vile Yahweh alivyokuwa ameagiza kwa mkono wa Musa.
9Kutoka kwa makabila la Yuda na Simoni, waliwapa nchi katika miji ifuatayo iliyoorodheshwa kwa majina.
10Miji hii walipewa wazawa wa Haruni, ambao walikuwa miongoni mwa koo za Wakohathi, ambao walitoka katika kabila la Lawi. Kwa kuwa upigaji wa kura ya kwanza uliwaangukiwa wao.
11Waisraeli waliwapatia Kiriathi Arba (Arba alikuwa ni baba wa Anaki), eneo hilo liliitwa pia Hebroni, katika nchi ya milima ya Yuda, pamoja na maeneo ya kulishia mifugo yaliyouzunguka mji.
12Lakini mashamba ya mji na vijiji vyake vilikuwa tayari ameshapewa Kalebu mwana Yefune, kama mali yake.
13Na kwa wana wa Haruni kuhani, waliwapa Hebroni pamoja na eneo lake la kulishia mifugo ambao ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia na Libna pamoja na maeneo ya kulishia mifugo.
14Na Yatiri pamoaja na maeno yake ya kuchungia, na Eshitemoa pamoja na maeneo yake ya malisho.
15Lakini pia waliwapa Holoni pamoja na maeneo yake ya malisho, Debiri pamoja na maeneo yake ya malisho,
16Aini pampoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. Ilikuwa ni miji kumi na tisa ambayo walipewa kutoka katika makabila haya mawilil.
17Kutoka katika kabilala Benyamini walipewa Gibea pamoja na maeneo yake ya malisho, na Geba pamoja na maeneo yake ya malisho,
18na Anathothi pamoja na maeneo yake ya malisho, na amoni pamoja na vitongoji vyake vinne.
19Miji waliyopewa makuhani, wana wa Haruni, ilikuwa ni miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumlisha na maeneo yake ya malisho.
20Na kwa ajili ya sehemu ya familia ya Kohathi iliyosalia, wale Walawi walio wa familia ya Kohathi, walipewa miji kutoka katika kabila la Efraimu kwa kupiga kura.
21Walipewa Shekemu pamoja na maeneo yake ya malisho katika nchi ya milima ya Efraimu - mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia, na Gezeri pamoja na maeneo yake ya malisho,
22na Kibzaimu pamoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Horoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa miji minne kwa ujumla wake.
23Kutoka katika kabila la Dani, ukoo wa Kohathi ulipewa Elteke pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gibethoni pamoja na maeneo yake ya malisho, na
24Aijaloni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gathrimoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake.
25Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, ukoo wa Kohathi walipewa miji miwili - Taanaki pamoja na maeneo yake ya malisho na Gathirimoni pamoja na maeneo yake ya malisho.
26Kulikuwa na miji kumi kwa ujumla wake kwa ajili ya koo zilizosalia za Wakohathi, pamoja na maeneo yao ya malisho.
27Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, jamaa za Gershoni, ambazo hizi zilikuwa ni koo zingine za Walawi, zilipewa Golani katika Bashani pamoja na maeneo yao ya malisho, ni mji wa makimbilio kwa ajili ya mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia, sambamba na Beeshitera pamoja na maeneo yake ya malisho - ilikuwa miji miwili kwa ujumla.
28Koo za Gershoni zilipewa pia miji minne kutoka kwa kabila la Isakari - Kishoni sambamba na maeneo yake ya malisho, Daberathi pamoja na maeneo yake ya malisho,
29Yarmuthi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Engnimu pamoja na maeneo yake ya malisho.
30Kutoka katika kabila la Asheri, walipewa miji minne kwa ujumla - Mishali pamoja na maeneo yake ya malisho, Abdoni pamoja na maeneo yake ya malisho,
31Helikathi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Rehobu pamoja na maeneo yake ya malisho.
32Kutoka kwa kabila la Nafutali, nasaba za Gershoni walipewa miji mitatu kwa ujumla - Kedeshi katika Galilaya pamoja na maeneo yake ya malisho, ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia; na Hamothidori pamoja na maeneo yake ya malisho, na Kartani pamoja na maeneo yake ya malisho.
33Kulikuwa na miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumuisha na maeneo yake ya malisho, kwa ajili ya koo za Gershoni.
34Na kwa Walawi waliosalia, koo za Merari waliokuwa wamepewa kutoka katika kabila la Zabuloni: Yokneamu pamoa na maeneo yake ya marisho, Karta pamoja na maeneo yake ya malisho,
35Dimna pamoja na maeneo yake ya malisho, na Nahalali pamoja na maeneo yake ya malisho- ilikuwa ni miji minne kwa ujumla.
36Kwa mbari za Merari walipewa miji minne kutoka katika kabila la Rubeni: Bezeri pamoja na maeneo yake ya malisho, Yahazi pamoja na maene yake ya malisho,
37na Kedemothi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.
38Kutoka katika kabila la Gadi walipewa miji ya Ramothi katika Gileadi pamoja na sehemu zake za malisho - huu ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu mwenzake bila kukusudia - na Mahanaimu pamoja na sehemu zake za malisho.
39Koo za Merari zilipewa pia Heshiboni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Yazeri pamoja na malisho yake.
40Hii ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake. Hii yote ilikuwa ni miji ya koo kadhaa za Merari, ambao walitoka katika kabila la Lawi, miji kumi na miwili walipewa wao kwa kupiga kura.
41Miji waliyopewa Walawi kutoka katikati ya nchi iliyomilikiwa na watu wa Israeli ilikuwa miji arobaini na nane, kujumuisha na sehemu za malisho yao.
42Miji hii kila mmoja ulikuwa na maeneo yake ya malisho kwa kuuzunguka mji. Miji hii yote ilikuwa hivyo.
43Basi Yahweh aliwapa Israeli nchi yote ambayo aliwaapia baba zao kuwa atawapa. Waisraeli waliimiliki nchi na wakakaa humo.
44Kisha Yahweh akawapa pumziko kwa kila upande, kama tu alivyowaahidia baba zao. Hakuna hata adui mmoja atakayeweza kuwashinda. Yawhew aliwatia maadui wao wote mikononi mwao.
45Hakuna hata kitu kimoja miongoni kwa ahadi nzuri ambazo Yahweh alizisema kwa nyumba ya Israeli ambazo hazikutimia. Ahadi zote zilitimia.