Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua

Yoshua 22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa wakati huo, Yoshua aliwaita Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase.
2Aliwaambia, “Mmefanya kila kitu ambacho Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi. Mmeitii sauti yangu katika yote niliyowaagiza.
3Bado hamjawaacha ndugu zenu hawa kwa siku zote hizi, mpaka siku hii ya leo. Na mmetimiza wajibu unaotakiwa na amri za Yahweh Mungu wenu.
4Sasa Yahweh Mungu wenu amewapa pumziko ndugu zenu, kama alivyowaahidi. Hivyo basi, rudini na mwende katika hema zenu katika nchi mnayoimiliki, ambayo Musa mtumishi wa Yahweh aliwapeni katika upande mwingine wa Yordani.
5Lakini zingatieni kuzishika amri na sheria ambazo Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi, kumpenda Yahweh Mungu wenu, kutembea katika njia zake, kuzitunza amri zake, na kuambatana naye na kumwabudu yeye kwa moyo wenu wote na kwa roho zenu zote.
6Basi Yoshua akawabariki na kisha akawaacha waende zao, nao wakarudi katika hema zao.
7Na kwa nusu ya kabila la Manase, Musa alikuwa amewapa urithi katika Bashani, lakini kwa nusu ya kabila hilo, Yoshua aliwapa urithi karibu na ndugu zao katika nchi magharibi mwa Yordani. Yoshua aliwaaga waende katika hema zao; aliwabarikia,
8na kisha akawaambia, “Rudini katika hema zenu mkiwa na pesa nyingi, na mkiwa na mifugo mingi, pamoja na na fedha, na dhahabu, na shaba na chuma, na nguo nyingi. Gawaneni na ndugu zenu nyara mlizochukua kutoka kwa maadui zenu.
9Hivyo, wazawa wa Rubeni, wazawa wa Gadi na nusu ya kabila la Manase walirudi nyumbani, waliwaacha watu wa Isaeli hapo Shilo, ambayo imo ndani ya nchi ya Kanaani. Waliondoka wakaenda katika mkoa wa Gileadi, katika nchi yao, ambayo wao wenyewe waliimiliki, katika utiifu wa amri za Yahweh, kwa mkono wa Musa.
10Nao walipofika hapo Yordani iliyo katika nchi ya Kanaani, Warubeni na Wagadi na nusu ya kabila la Manase walijenga madhabahu karibu na Yordani, madhabahu kubwa na iliyotokeza na mashuhuri.
11Watu wa Israeli walisikia habari hizo na wakaseam, “Tazama! Watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wamejenga madhabahu mbele ya nchi ya Kanaani, huko Gelilothi, katika mkoa karibu na Yordani, katika upande ambao ni miliki ya watu wa Israeli.”
12Wakati watu wa Israeli waliposikia hivyo, kusanyiko lote la watu wa Israeli walikusanyika kwa pamoja huko Shilo ili wapande kupigana vita nao.
13Kisha watu wa Israeli walituma wajumbe kwa Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi. Walimtuma pia Finehasi mwana wa Eliezari, kuhani,
14na viongozi kumi pamoja naye, mmoja kutoka katika familia za mababa wa Israeli, na kila mmoja wao alikuwa ni kiongozi wa ukoo miongoni mwa watu wa Israeli.
15Walienda kwa watu wa Rubeni, Gadi, na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakawaambia:
16“Kusanyiko lote la Yahweh linasema kuwa, 'Ni jambo gani hili lisilo la uaminifu ambalo mmelitenda kinyume na Mungu wa Israeli, kwa kugeuka badala ya kumfuata Yahweh siku hii na kujijengea wenyewe madhabahu katika uasi kinyume na Yahweh katika siku hii?
17Je dhambi zetu huko Peori hazikututosha? Bado hata sasa hatujajitakasa wenyewe kwa dhambi hiyo. Kwa ajili ya dhambi ile lilikuja pigo kwa kusanyiko lote la Yahweh.
18Je, nanyi leo pia mwageuka na kuacha kumfuata Yahweh? Kama mtaasi kinyume na Yahweh leo, kesho atakuwa na hasira na kusanyiko lote la Israeli.

19Na kama nchi ambayo mnaimiliki imetiwa unajisi, basi mwaweza kuvuka katika nchi ambayo Sanduku la Yahweh lasimama na mjichukulie kwa ajili yenu umiliki miongoni mwetu. Hamtakiwi kuasi kinyume na Yahweh tu, wala kuasi kinyume chetu kwa kujenga madhabahu kwa ajili yenu wenyewe badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wa wetu.
20Je hakuwa Akani mwana wa Zera aliyeivunja imani kwa vitu vile ambavyo vilikuwa vimetunzwa kwa ajili ya Mungu? Na je ghadhabu ya Mungu haikushuka kwa watu wote wa Israeli? Mtu yule hakuangamia peke yake kwa uovu wake.
21Kisha makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wakawajibu wazee wa koo za Israeli:
22“Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yeye anajua, na Israeli naijue yenyewe! Kama ilikuwa ni katika uasi au katika kuvunja imani kinyume na Yahweh, msituache hai katika siku hii ya leo
23kwa ajili ya kujenga madhabahu ili tugeuka na kuacha kumfuata Yahweh. Kama tumejenga madhabahu hii ili kutoa juu yake sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, au sadaka ya amani, basi Yahweh na atuadhibu.
24La hasha, tulifanya hivyo kwa sababu ya hofu kwamba katika siku zijazo watoto wenu wanaweza kuwaambia watoto wetu, 'Mna nini ninyi na Yahweh, Mungu wa Israeli?
25Kwa kuwa Yahweh ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi. Ninyi watu wa Rubeni na watu wa Gadi, hamna kitu chochote naYahweh.' Na kwa hali hiyo, watoto wenu wanaweza kuwafanya watoto wetu waacha kumwabudu Yahweh.
26Basi tukasema, 'Hebu na tujenge sasa madhabahu, si kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa wala si kwa sadaka yoyote ile,
27ila iwe ni ushahidi kati yetu na ninyi, na kati ya kizazi chetu baada yetu, kwamba tutafanya ibada ya Yahweh mbele yake, pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa na dhabihu zetu na sadaka zetu za amani, ili kwamba watoto wenu wasiweze kuwaambia watoto wetu katika siku zijazo kuwa, “Hamna sehemu katika Yahweh.”'
28Hivyo tukasema, 'kama hili litasemwa kwa kwetu au kwa watoto wetu katika siku zijazo, tutasema, “Tazama! Huu ni mfano wa madhabahu ya Yahweh, ambayo mababu zetu waliifanya, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala si kwa dhabihu, bali kwa ajili ya ushahidi kati yetu ninyi.”
29Na iwe mbali nasi kwamba tunataka kugeuka kinyume na Yahweh, na kuacha kumfuata yeye kwa kujenga madhabahu kwa ajili sadaka ya kuteketezwa, na kwa sadaka ya nafaka, au kwa dhabihu, badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wetu ambayo iko mbele ya hema la kukutania.'”
30Finehasi kuhani na viongozi wa watu, ambao ni wakuu wa koo za Waisraeli ambao walikuwa pamoja naye, waliposikia maneno amabayo watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, kwamba yalikuwa ni mazuri machoni pao.
31Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani aliwaambia watu wa Rubeni, Gadi na Manase, “Leo tumejua kwambaYahweh yuko miongoni mwetu, kwa kuwa hamjatenda uvunjaji wa imani kinyume naye. Sasa, mmewaokoa watu wa Israeli kutoka katika mkono wa Yahweh.”
32Kisha Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani, na viongozi walirudi kutoka kwa Warubeni na Wagadi, kutoka katika nchi ya Gileadi, na kurudi katika nchi ya Kanaani, kwa watu wa Israeli, na waliwaletea taarifa.
33Taarifa yao ilikuwa nzuri katika macho ya watu wa Israeli. Watu wa Israeli walimbarikia Mungu na hawakuendelea kusema tena juu ya kuinua vita dhidi ya Warubeni na Wagadi, ili kuiharibu nchi ambayo walikuwa wanaishi.
34Warubeni na Wagadi waliita ile madhabahu “Ushahidi,” kwa kuwa walisema, “Ni ushahidi miongoni mwetu kuwa Yahweh ni Mungu.”