Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua

Yoshua 20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Baada ya hayo, Yahweh akamwambia Yoshua,
2“Waambia watu wa Israeli, na kusema, 'Chagueni miji ya makimbilio ambayo niliwaambia kupitia kwa Musa.
3Fanyeni hivi ili mtu akiua mtu bila kukusudia aweze kwenda huko. Miji hii itakuwa ni sehemu ya kukimbilia kutoka kwa mtu yeyote yule anayetaka kulipiza kisasi kwa damu ya mtu aliyeuliwa.
4Atakimbilia kwa mji mmoja miongoni mwa miji hiyo na atasimama mlangoni mwa lango la mji, na ataeleza kesi yake kwa wazee wa mji ule. Kisha watamwingiza ndani ya mji na watampatia sehemu yake ya kuishi miongoni mwao.
5Na kama mtu akija akataka kulipiza kisasi kwa damu ya mtu yule ambaye aliuliwa, ndipo watu wa mji hawatatakiwa kumtoa kwa wenye mamlaka mtu huyo aliyeua. Hawaruhusiwi kufanya hivyo kwasababu alimwua jirani bila kukusudia na hakuwa na chuki naye hapo awali.
6Ni lazima akae katika mji ule mpaka pale atakapokuwa amesimama mbele ya kusanyiko kwa ajili ya kuhukumiwa, hadi pale atakapokufa mtu yule anayetumika katika nafasi ya kuhani mkuu katka siku hizo. Na kisha mtu yule aliyeua bila kukusudia aweza kurudi nyumbani kwake, katika mji ule ulikotoka.
7Kwahiyo, Waisraeli wakaichaguia Kedeshi iliyoko Galilaya katika nchi ya milima ya Nafutali, Shekemu katika nchi ya milima ya Efraimu, na Kiriathi Arba (ambayo ndio Herbroni) katika nchi ya milima ya Yuda.
8Katika ng'ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko, walichagua mji wa Bezeri huko nyikani katika nyanda za kabila la Rubeni; na Ramothi Gileadi kutoka kabila la Gadi; na Golani katika Bashani, kutoka katika kabila la Manase.
9Hii ni miji iliyochaguliwa kwa ajili ya watu wote wa Israeli na kwa ajili ya wageni wanaoishi miongoni mwao, ili kwamba mtu yeyote amwuaye mtu bila kukusudia aweza kukimbilia huko kwa ajili ya kupata usalama. Mtu huyu hatakufa kwa mkono wa mtu yule anayetake kulipiza kisasi cha damu iliyomwagwa, mpaka hapo kwanza mtuhumiwa atakaposimama mbele ya kusanyiko la watu.