Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua

Yoshua 8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahweh akamwambia Yoshua, “Usiogope; usivunjike moyo. Chukua pamoja nawe watu wa vita. Pandeni kwenda Ai. Tazama nimemtia mkononi mwako mfalme wa Ai, watu wake, mji wake na nchi yake.
2Mtafanya hivyo pia huko Ai na mfalme wake kama mlivyofanya kwa Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mtachukua nyara na mifugo kwa ajili yenu. Pangeni mashambulizi ya uviziaji nyuma ya mji.”
3Basi Yoshua aliinuka na akawachukua kwenda Ai watu wote wa vita. Kisha Yoshua akachagua watu elfu thelathini - wenye nguvu na ujasiri - na aliwatuma waende wakati wa usiku.
4Aliwaamuru, “Tazama, mtalala katika hali ya mashambulizi ya uviziaji dhidi ya mji, kwa nyuma yake. Usiende mbali sana na mji, lakini ninyi nyote muwe tayari.
5Mimi pamoja na watu wote walio pamoja nami tutaukaribia mji. Na wakati watakapokuja kutushambulia sisi, tutawakimbia kama tulivyofanya hapo mwanzo.
6Watatoka nje watukimbize mpaka hapo tutakapokuwa tumewavuta mbali sana na mji, watasema, “Wanatukimbia kama walivyofanya mara ya mwisho.' Hivyo tutawakimbia na kwenda mbali.
7Kisha mtapanda kutoka sehemu mliyojificha, na mtauteka mji. Yahweh Mungu wenu atawapa mkononi mwenu.
8Tazama nimewaamuru, mtakapouteka mji, mtauchoma moto. Mtayafanya haya wakati mtakapotii agizo lililotolewa katika neno la Yahweh.”
9Yoshua akawatuma, na wakaenda sehemu ya uviziajia, na wakajificha kati ya Betheli na Ai sehemu ya magharibi ya Ai. Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku ule.
10Yoshua aliamka asubuhi na mapema na akawaandaa tayari wanajeshi wake, Yoshua na wazee wa Israeli walishambuliwa watu wa Ai.
11Watu wote wa vita waliokuwa pamoja naye walipanda na kuukaribia mji. Walisogea karibu na mji na wakapiga kambi sehemu ya kasikazini mwa Ai. Kulikuwa na bonde kati yao na Ai.
12Alichukua watu wapatao elfu tano hivi na akawaweka katika hali ya kuvizia katika upande wa magharibi mwa mji kati ya Betheli na Ai.
13Waliwapanga wanajeshi wote, jeshi kuu katika upande wa kasikazini mwa mji, na walinzi wa nyuma upande wa magharibi mwa mji. Yoshua alilala bondeni usiku ule.
14Na ilikuwa alipoona hilo mfalme wa Ai, yeye pamoja na jeshi lake, waliamka asubuhi na mapema na walitoka kwa haraka kwenda kuwashambulia Israeli katika eneo linalokabili bonde la Mto Yordani. Hakujua kuwa kulikuwa na shambulizi la kuvizia lilikuwa linasubiria kushambulia kutokea kwa nyuma ya mji.
15Yoshua na Waisraeli wote walikubali wenyewe kushindwa mbele yenu, na wakakimbia kuelekea nyikani.
16Watu wote waliokuwa kwenye mji waliitwa kwa pamoja waende mbele yao, na walienda mbele ya Yoshua na kwa jinsi hiyo walivutwa mbali na mji.
17Hapakuwa na mtu mme aliyesalia Ai na Betheli ambaye alikuwa hajaenda nje kuwafuatilia waisraeli. Na walipokuwa wanawafuatilia Waisraeli, Wakatoka na waliuacha mji wazi.
18Yahweh akamwambia Yoshua, “Nyosha mkuki huo ulio mkononi mwako kuelekea Ai, kwa kuwa nitaitia Ai mikononi mwako.” Yoshua akaunyosha mkuki uliokuwa mkononi mwake kuuelekea mji.

19Wanajeshi waliojificha katika hali ya kuvizia walitoka upesi katika eneo lao mara tu alipounyosha mkono wake. Walikimbia mbio na kuuingia mji na kuuteka. Na kwa haraka wakauchoma moto mji.
20Watu wa Ai waligeuka na kuangalia nyuma. Waliona moshi kutoka katika mji ukipanda kwenda angani, na hawakuweza kutoroka kwa njia hii au ile. Kwa kuwa wanajeshi wa Israelei waliokuwa wamekimbia katika nyika, sasa walirudi kuwakabili wale waliokuwa wanawafuatilia.
21Na wakati Yoshua na Israeli wote walipoona kuwa wale watu wa kuvizia wameuteka mji kwa ule moshi uliokuwa ukipanda, waligeuka nyuma na kuwaua watu wa Ai.
22Na wanajeshi wengine wa Israeli, wale waliokuwa wameingia ndani ya mji, walitoka nje ili kuwashambulia. Hivyo, watu wa Ai walikamatwa katikati ya majeshi ya Israeli, baadhi katika upande huu na wengine katika upande ule.
23Lakini walimhifadhi mfalme wa Ai, ambaye walimteka akiwa hai, na kisha wakamleta kwa Yoshua.
24Ilikuwa baada ya Israeli walipokuwa wamemaliza kuuwaua wenyeji wote wa Ai katika uwanda kariibu na nyika mahali walipowafuata, na baada ya wao wote, hata yule wa mwisho, walipokuwa wamekwisha kulala kwa ncha ya upanga, Waisraeli wote walirudi Ai. Waliuteka mji kwa ncha ya upanga.
25Wale wote walikufa siku hiyo walikuwa watu elfu kumi na mbili elfu, wanaume na wanawake, wote ni watu wa Ai.
26Yoshua hakuukunja mkono wake ambao alikuwa ameunyosha huku akishikilia mkuki wake, mpaka pale alipowateketeza kabisa watu wote wa Ai.
27Waisraeli walichukua tu wanyama na nyara kutoka katika mji kwa ajili yao wenyewe, kama Yahweh alivyokuwa amemwagiza Yoshua.
28Yoshua aliichoma Ai na kuigeuza kuwa kichuguu cha mapango. Ni mahali palipoachwa ukiwa hata leo.
29Alimtundika mfalme wa Ai juu ya mti mpaka jioni. Na jua lilipokuwa linaenda kuzama, Yoshua aliwaagiza na wakautoa mwili wa mfalme wakaushusha chini ya mti na kuutupa mbele ya malango ya mji. Huko wakaweka kichuguu kikubwa cha mawe juu yake. Kichuguu hicho kimebaki huko hata leo.
30Kisha Yoshua akajenga madhabahu kwa Yahweh, Mungu wa Israeli katika Mlima wa Ebali,
31kama vile Musa mtumishi wa Yahweh alivyowaagiza watu wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Musa: “Madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna mtu yeyote aliyetumia zana ya chuma.” Na allimtolea Yahweh sadaka ya kuteketezwa juu yake na wakatoa sadaka ya amani.
32Na huko aliandika juu ya mawe nakala ya sheria za Musa mbele ya watu wa Israeli.
33Waisraeli wote, wazee wao, maafisa, na waamuzi wao walisimama katika sehemu mbili za sanduku mbele ya makuhani na Walawi ambao hulibeba sanduku la Agano la Yahweh - wageni pamoja na wazalia, nusu yao walisimama mbele ya Mlima Gerizimu na nusu walisimama mbele ya Mlima Ebali. Waliwabariki watu wa Israeli kama Musa mtumishi wa Yahweh alivyowaagiza hapo mwanzo.
34Baada ya hayo, Yoshua alisoma maneno yote ya sheria, baraka na laana, kama zilivyoandikwa katika kitabu cha sheria.
35Halikusalia hata neno moja katika yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua ambalo halikusomwa mbele ya kusanyiko la Waisraeli lilojumuisha wanawake, watoto wadogo na wageni walioishi miongoni mwao.