Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua

Yoshua 15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ugawanaji wa nchi kwa kabila la watu wa Yuda, walipewa kwa kufuatana na koo zao, kutoka upande wa kusini hadi mpaka wa Edomu, pamoja na nyika ya Sini iliyokuwa mbali sana kuelekea kusini.
2Mpaka wao wa upande wa kusini ulianzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ghuba iliyokabili upande wa kusini.
3Mpaka wao mwingine ulielekea upande wa kusini wa mlima wa Akrabimu na kupita kuelekea Sini, na kupanda upande wa Kadeshi Barnea, karibu na Hezroni, hadi Addari mahali ambapo ulipinda kuelekea Karika.
4Ulipita katika Azimoni, kuelekea kijito cha Misri, na mwisho ulikuwa katika bahari. Huu ulikuwa ni mpaka wa kusini.
5Mpaka wa mashariki ulikuwa ni Bahari ya Chumvi, katika mdomo wa Yordani. Mpaka wa upande wa kasikazini ulianzia katika ghuba ya bahari katika mdomo wa Yordani.
6Ulielekea mpaka Bethi Hogla na ulipita kaskazini mwa Bethi Araba. Kisha ulipanda hata JIwe la Bohani mwana wa Rubeni.
7Basi mpaka ule ulienda hadi Debiri kutoka katika bonde la Akori, kuelekea upande wa kasikazini, kuendelea hadi Giligali, ambayo iko mkabala na mlima Adumimu, iliyo upande wa kusini wa bonde. Kisha mpaka uliendelea hata katika chemichemi za Eni Shemeshi na kufika Eni Rogeli.
8kisha mpaka ulishuka hadi bonde la Beni Hinomu kuelekea upande wa kusini wa mji wa Wayebusi (ambao ni Yerusalemu). Kisha ulipanda hata katika mlima ulio juu ya bonde la Hinomu, katika upande wa magharibi, ulio mwishoni mwa bonde la Refaimu katika upande wa kasikazini.
9Kisha mpaka ulitanuka kutoka katika kilele cha milima hata chemichemi ya Nefutoa, na ulipanda kutoka hapo kuelekea miji ya Mlima Efroni. Kisha mpaka ulipiga kona kuelekea Baala (ambao ndio Kiriathi Yearimu).
10Baadaye mpaka ulizunguka kuelekea magharibi mwa Baala kukabili Mlima Seiri, na kupita kufuata upande wa Mlima wa Yearimu katika upande wa kasikazini (ambao ndio Kesaloni), ulienda chini hadi Bethi Shemeshi na kuvuka hata ng'ambo ya Timna.
11Mpaka uliendelea karibu na mlima wa kasikazini mwa mlima wa Ekroni, na kisha ukakata kona kuzunguka Shikeroni na kupita kuelekea sambasamba na Mlima Baala, kutoka hapo uliendelea hadi Yabneeli. Mpaka ule ulikomea katika bahari.
12Mpaka wa magharibi ulikuwa Bahari Kuu na katika ukanda wa pwani yake. Huu ndio mpaka uliozunguka kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo.
13Katika kulitunza agizo la Yahweh kwa Yoshua, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune mgao wa nchi ya. miongoni mwa kabila la Yuda, alimgawia nchi Kiriathi Arba, ambayo ndio Hebroni (Arba alikuwa ni baba wa Anaki).
14Kalebu aliwafukuzia mbali wana watatu wa Anaki: Sheshai, Ahimani na Talmai, wazawa wa Anaki.
15Alipanda kutoka pale kinyume cha wenyeji wa Debiri (Debiri hapo mwanzo iliitwa Kiriathi Seferi).
16Kalebu akasema, “Mtu atakayeishambulia Kiriathi Seferi na kuiteka, nitampa binti yangau, Akisa, awe mke wake.
17Wakati huo Othinieli mwana wa Kenazi, kaka yake na Kalebu, aliuteka mji, na Kalebu alimpatia Akisa, binti yake awe mke wake.
18Mara baada ya hayo, Akisa alienda kwa Othinieli na alimsihi amwombe baba yake shamba. Na mara aliposhuka kutoka katika punda wake, Kalebu alimwambia Akisa, “Unataka nini?”

19Akisa akamjibu, “Nifanyie neema. Kwa kuwa umeshanipa nchi ya Negevu, nipe pia baadhi ya chemichemi za maji.” Na Kalebu alimpa chemichemi ya juu na chemichemi ya chini.
20Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Yuda, waliopewa kufuatana na koo zao.
21Miji iliyo mali ya kabila la Yuda katika upande wa kusini, kuelekea mpaka wa Edomu, ilikuwa ni Kabzeeli, Eda, Yaguri,
22Kina, Dimona, Adada,
23Kadeshi, Hazor, Ithinani,
24Zifu, Telemu, Bealothi.
25Hazori Hadata, Keriothi Hezroni (mji huu ulijulikana kama Hazori),
26Amamu, shema, Molada,
27Hazari Gada, Heshimoni, Bethi Peleti,
28Hazari Shuali, Beerisheba, Biziothia.
29Baala, Limu, Ezemu,
30Eltoladi, Kesili, Horma,
31Ziklagi, Madimana, Sansana,
32Lebaothi, Shilihimu, Aini, na Rimoni. Miji hii ilikuwa ishirini na tisa kwa ujumla, kujumlisha na vijiji vyake.
33Katika nchi iliyo chini ya mlima upande wa magharibi, kulikuwa na miji ya Eshtaoli, Zora, Ashina,
34Zanaoa, Eni Ganimu, Tapua, Enamu,
35Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka,
36Shaaraimu, Adithaimu, na Gedera (ambayo ndio Gederothaimu). Hesabu ya miji hii ilikuwa ni kumi na nne, pamoja na vijiji vyao.

37Zena, Hadasha, Migidagadi,
38Dileani, Mizipa, Yokitheeli,
39Lakishi, Bozikathi, Egloni.
40Kaboni, Lahmamu, Kitilishi,
41Gederothi, Bethi Dagoni, Naama, Makeda. Hesabu ya miji hii ilikuwa kumi na sita, kujumlisha na vijiji vyao.
42Libna, Etheri, Ashani,
43Ifuta, Ashina, Nezibu,
44Keila, Akizibu, na Maresha. Hii ilikuwa ni miji tisa, kujumlisha na vijiji vyao.
45Ekroni, pamoja na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka;
46kutoka Ekroni kuelekea Bahari Kuu, makazi yote ambayo yalikuwa karibu na Ashidodi, pamoja na vijiji vyake.
47Ashidodi, na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; Gaza na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; hata kufika kijito cha Misri, na kuelekea Bahari Kuu pamoja na ukanda wake wa pwani.
48Katika nchi ya milima, kuna miji ya Shamiri, Yatiri, Soko,
49Dana, Kiriathi Sana (ambayo ndio Debiri),
50Anabu, Eshitemo, Animu,
51Gosheni, Holoni, na Gilo. Hii ilikuwa ni miji kumi na moja, kujumuisha na vijiji vyake.
52Arabu, Duma, Ehani,
53Yanimu, Bethi Tapua, Afeka,
54Humta, Kiriathi Arba (ambayo ndio Hebroni), na Ziori. Hii ilikuwa miji tisa, pamoja na vijiji vyake.

55Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,
56Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,
57Kaini, Gibea, na Timna. Hii ilikuwa ni miji kumi, kujumuisha na vijiji vyake.
58Halhuli, Bethi Zuri, Gedori,
59Maarathi, Bethi Anothi, na Elitekoni. Hii ilikuwa miji sita, pamoja na vijiji vyake.
60Kiriathi Baali (ambayo ndio Kiriathi Yearimu), na Raba. Hii ilikuwa ni miji miwili, pamoja na vijiji vyake.
61Katika nyika, kulikuwa na miji ya Bethi Araba, Midini, Sekaka,
62Nibushani, mji wa chumvi, na Eni Gedi. Hii ilikuwa miji, pamoja na vijiji vyao.
63Lakini kwa Wayebusi, wenyeji wa Yerusalemu, kabila la Yuda halikuweza kuwafukuza, na hivyo, Wayebusi wanaishi pamoja na kabila la Yuda hadi leo hii.