Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 1

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, na siku ya tano ya mwezi, ikawa kuhusu kwamba nilikuwa nikiishi miongoni mwa wafungwa karibu na Kebari Kanali. Mbingu zilifunguka, na kuona maono ya Mungu.
2Katika siku ya tano katika mwezi huo-ilikuwa mwaka wa tano wa utumwani wa Mfalme Yehoyakini-
3Neno la Yahwe likamjia Ezekieli mwana wa Buzi kuhani, katika nchi ya Wakaldayo karibu na Keberi Kanali, na mkono wa Yahwe ulikuwa juu yake hapo.
4Kisha nikaona, kulikuwa na upepo wa dhoruba unakuja kutoka kaskazini; wingu kubwa pamoja na moto wa nuru ndani yake na kung'aa ukizunguka ndani yake, na moto ulikuwa na rangi ya kaharabu ndani ya hilo wingu.
5Katikati kulikuwa na viumbe vinne vinavyofanana. Mwonekano wao ulikuwa hivi: walikuwa wanamfanano wa mtu,
6lakini walikuwa na sura nne kila mmoja, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne.
7Miguu yao ilikuwa imenyooka, lakini nyayo za miguu yao zilikuwa kama kwato za ndama zilizokuwa zinang'aa kama shaba iliyosuguliwa.
8Bado walikuwa na mikono ya binadamu chini ya mabawa yao chini kwenye pande zote nne. Kwa wote wanne, nyuso zao na mabawa vilikuwa hivi:
9mabawa yao yalikuwa yameungana na kiumbe kingine, na hawakurudi walipokuwa wameenda; badala yake, kila mmoja alienda mbele.
10Mfanano wa nyuso zao ulikuwa kama uso wa mwanadamu. Wanne hao walikuwa na uso wa simba kwa upande wa kuume. Hao wanne pia walikuwa na uso wa tai.
11Nyuso zao zilikuwa hivyo, na mabawa yao yalikuwa yametawanyika juu, hivyo basi kila kiumbe kilikuwa na jozi ya za mabawa yaliyokuwa yameshikamana na bawa la kiumbe kingine, na pia jozi za mabawa yaliyokuwa yamefunika miili yao.
12Kila mmoja alienda mbele, hivyo basi popote Roho alipowaelekeza kwanda, walienda bila kurudi.
13Kama kwa mfanano wa hao viumbe hai, mwonekano wao ulikuwa ni kama kuchoma kaa la moto, kama mwonekano wa nuru; mng'ao wa moto pia ulihama karibu na miongoni mwa viumbe, na kulikuwa na nuru za radi.
14Hao viumbe hai vilikuwa vikihama mbio mbele na nyuma, na walikuwa na mwonekano wa radi!
15Kisha nikawatazama wale viumbe hai; kulikuwa na gurudumu moja juu ya aridhi kando ya vile viumbe hai.
16Huu ndio ulikuwa mwonekano na umbo wa hizo gurudumu: kila gurudumu lilikuwa kama zabarajadi, na manne hayo yalikuwa na mfano mmoja; mwonekano wao na umbo vilikuwa kama gurudumu lililoungana na jingine.
17Wakati yale magurudumu yalipokuwa yakitembea, yalienda bila kurudi kwenye mwelekeo wowote viumbe vilipokuwa vimeelekea.
18Kama kwa upande kingo, walikuwa warefu na wakutisha, kwa upande kingo kulikuwa na macho yamezunguka kote.

19Popote vile viumbe hai vilipokuwa vikielekea, yale magurudumu yalielekea karibu nao. Wakati vile viumbe hai vilipoinuka kutoka kwenye nchi, na yale magurudumu yaliinuka pia.
20Popote Roho alipokwenda, walikwenda, na yale magurudumu yaliinuka karibu nao, roho wa kiumbe hai ilikuwa magurudumu.
21Popote vile viumbe vilipoelekea, magurudumu pia yalielekea huko; na wakati wale viumbe viliposimama hata hivyo, magurudumu yalisimama bado; wakati viumbe viliposimama kutoka kwenye nchi, magurudumu yalisimama karibu nao, kwa sababu yule roho wa wale viumbe alikuwa kwenye magurudumu.
22Juu ya vichwa vya wale viumbe hai kulikuwa na mfanano wa anga la kutanuka; ilikuwa inang'aa kama mfano wa barafu juu ya vichwa vyao.
23Chini ya anga, kila mabawa ya kiumbe kimoja yalinyooshwa mbele na kugusana kila mabawa na kiumbe kimoja. Pia kila kiumbe hai kilikuwa na jozi moja kwa ajili ya kujifunika vyenyewe; kila kimoja kilikuwa na jozi moja kwa ajili ya kujifunika mwili wake mwenyewe.
24Kisha nikasikia sauti ya mabawa yao. Kama mlio wa maji mengi. Kama sauti ya mwenye enzi popote walipoelekea. Kama sauti ya jeshi. Popote pale waliposimama, walishusha mabawa yao.
25Sauti ikaja kutoka juu ya anga juu ya vichwa vyao popote waliposimama na kushusha mabawa yao.
26Juu ya anga juu ya vichwa vyao kulikuwa na mfanao wa kiti cha enzi ambacho kilikuwa na mwonekano wa jiwe la samawati, na juu mfano wa kiti cha enzi kilifanana kama mwonekano wa mwanadamu.
27Nikaona umbo lenye mwonekano wa chuma chenye kung'aa pamoja na moto ndani yake kutoka kwenye mwonekano wa juu ya nyonga zake juu; Nikaona kutoka kwenye mwonekano wa nyonga zake upande wa chini mwonekano wa moto na mng'ao umezunguka kote.
28Kama mwonekano wa upinde wa mvua kwenye mawingu katika siku ya mvua ulikuwa na mwonekano wa taa iliyowaka imeizunguka. ulikuwa na mwonekano unaofanana na utukufu wa Yahwe. Wakati nilipouona, nilihisi kwenye uso wangu, na nikasikia sauti ikiongea.