Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 31

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa tatu, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
2“Mwanadamu, mwambie Farao, mfalme wa Misri, na watu wake wanaomzunguka, 'Katika ukuu wako, je! wewe ni kama nani?
3Tazama! Ashuru ilikuwa mwerezi katika Lebanoni pamoja na matawi mazuri, yakitoa kivuli kwenye msitu, na mirefu katika kimo, na matawi yalitengeneza kilele cha mti wake.
4Maji mengi yaliufanya kuwa mrefu; maji ya chini yaliufanya kuwa mkuba. Mito ilitiririka sehemu zake zote, kwa kuwa mifereji yake ilitoa kuelekea kwenye miti yote katika shamba.
5Kimo chake kikubwa kilikuwa zaidi kuliko miti mingine yote katika shamba, na matawi yake yakawa mengi; matawi yake yalikuwa marefu kwa sababu ya maji mengi yalipokuwa yakikua.
6Kila ndege wa mbinguni alitengeza kiota kwenye matawi yake, wakati kila kiumbe hai cha shamba kilizaa mtoto chini ya tawi. Mataifa mengi yote yaliishi chini ya kivuli chake.
7Kwa kuwa ulikuwa uzuri katika ukuu wake na kimo cha matawi yake, kwa kuwa mizizi yake ilikuwa katika maji mengi.
8Mierezi katika bustani ya Mungu haikuweza kuwa sawa nayo. Hakuna miongoni mwa miti ya mivinje iliyofanana matawi yake, na miti ya miamori haikuweza kuwa sawa na majani yake. Hapakuwa na mti mwingine katika bustani ya Mungu ulikuwa kama huo katika uzuri wake.
9Nimeufanya kuwa mzuri pamoja na matawi yake mengi na miti yote ya Edeni iliyokuwa katika bustani ya Mungu ilimwonea wivu.
10Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu ilikuwa mirefu kwa kina, na imekiweka kilele chake kati ya matawi yake, moyo wake umeinua kwa sababu ya urefu wake.
11Nimeuweka kwenye mikono ya yeye mwenye uweza wa mataifa, kuishughulikia kulingana na yale maovu anayostahili. Nimeufukuza.
12Wageni waliokuwa wakiogofya wa mataifa yote wameikatilia mbali kuiacha ife. Matawi yake yameanguka kwenye milima na mabonde yote, na matawi yake yameanguka katika mito yote ya nchi. Kisha mataifa yote juu ya nchi wakatoka nje kutoka chini ya kivuli na kwenda zao wakamwacha.
13Ndege wa agani watapumzika kwenye shina la mti ulioanguka, na kila mnyama wa shambani atakuja kwenye matawi yake.
14Hii litokea ili kwamba pasiwe na miti mingine itakayopandwa karibu na maji yatang'oa majani yake hata kwenye kina cha miti mirefu, na kwamba hakuna miti mingine itakayomea karibu na maji itakayofikia kwenye hicho kina. Wote wametolewa kufa, chini ya nchi, miongoni mwa watoto wa binadamu, pamoja na wale washukao chini.
15Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku wakati mkangazi uliposhuka chini nilileta maombolezo kwenye dunia. Niliyafunika maji ya chini juu yake, nikayarudisha maji ya bahari. Nilizuia maji makuu, nikaleta maombolezo hata Lebanoni kwa ajili yake. Hivyo miti yote ya shambani ikaomboleza kwa sababu yake.
16Nimeleta tetemeko kwa mataifa wa sauti ya kuanguka kwake, wakati nitakapomtupa chini mpaka kuzimu pamoja na wale walioenda chini kwenye shimo. Hivyo niliitia moyo miti ya Edeni yote katika pande zote za nchi. Hii ilikuwa imechaguliwa na miti iliyokuwa bora ya Lenanoni; miti iliyokunywa maji.
17Kwa kuwa walikwenda chini pia pamoja nayo hata kuzimu, kwa wale waliokuwa wameuawa kwa upanga. Kulikuwa na jeshi lake imara, yale mataifa yalikuwa yakiishi kati kivuli chake.
18Umefanana na nani hivi katika utukufu na ukuu kati ya mti wa Edeni? Kwa kuwa utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni hata pande zote nne za dunia miongoni mwa wasiotahiriwa; utaishi pamoja na watu wake wote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavy.”