Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
2“Mwanadamu, sema hivi kwa watu wako; waambie, 'Nitakapoleta upanga juu ya nchi, kisha watu wa hiyo nchi wakamchukua mtu mmoja kutoka mingoni mwao na kumfanya awe mlinzi wao.
3Atazamapo kwa upanga kama unakuja juu ya nchi, na apige tarumbeta kuwaonya watu!
4Kama watu wakisikia sauti ya tarumbeta lakini bila kusikia, na kama upanga ukija na kuwaua, kisha damu ya kila mmoja iko juu ya kichwa chake mwenyewe.
5Kama mtu akisikia sauti ya tarumbeta na hakusikiliza, damu yake iko juu yake; lakini kama akisikia, ataokoa maisha yake mwenyewe.
6Bali, kama mlinzi akiona upanga unakuja, lakini kama asipopiga tarumbeta, pamoja na matokeo kwamba watu hawajaonywa, na kama upanga ukija na kuchukua uhai wa mtu yeyote, kisha yule mtu akafa kwenye dhambi yake mwenyewe, lakini nitaitaka damu yake kutoka mlinzi.'
7Sasa wewe mwenyewe, mwanadamu! Nimekufanya kuwa mlinzi kwa ajili ya nyumba ya Israeli; utasikia maneno kutoka kinywani mwangu na uwaonye badala yangu.
8Kama nikimwambia mtu mwovu, 'Mwovu, hakika utakufa!' lakini kama hutangazi hivi ili kwa ajili ya kumuonya mtu mwovu kuhusu hii njia, kisha huyo mtu mwovu atakufa katika dhambi yake, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako!
9Lakini wewe, kama ukimwonya mwovu kuhusu hii njia, hivyo basi anaweza kurudi kutoka hiyo, na kama kama asipogeuka kutoka njia yake, kisha atakufa katika dhambi yake, lakini wewe mwenyewe utakuwa umeokoa maisha yako.
10Basi wewe, mwanadamu, sema kwa nyumba ya Israeli, 'Mnasema hivi, Makosa yetu na dhambi zetu zi juu yetu, na tunadhoofika kwa ajili yao! Je! tutaishije?”'
11Waambie, 'Kama niishivyo-asema Bwana Yahwe-sifurahii kifo cha mwovu, kwa kuwa kama mwovu akitubu kutoka njia yake, kisha ataishi! Tubu! Tubu kutoka njia zako mbaya! Kwa nini mnataka kufa, nyumba ya Israeli?'
12Hivyo basi wewe, mwanadamu, waambe watu wako, 'Haki ya mwenye haki haitamwokoa kama akikosa! Uovu wa mtu mwovu hautamfanya kuangamia kama akitubu dhambi zake! Kwa kuwa mtu mwenye haki hataweza kuishi kwa sababu ya haki yake kama akikosa.
13Kama nikisema kwa mwenye haki, “Hakika ataisha!” na kama akiamini katika haki yake na kisha akafanya udhalimu, sitokumbuka haki yake yoyote. Atakufa kwa ajili ya uovu alioufanya.
14Hivyo kama nikisema kwa mwovu, “Utakufa hakika,” lakini kama akitubu kutoka kwenye dhambi zake na kufanya yaliyo halali na haki-
15kama akirudisha dhamana ambayo aliyomnyang'anya, au kama akirudisha alichokipoteza, na kama akitembea katika amri zitoazo uhai na bila kufanya dhambi-kisha ataishi hakika. Hatakufa.
16Dhambi alizozifanya hazitakumbukwa kwa ajili yake. Ametenda halali na haki, na hivyo, ataishi hakika!
17Lakini watu wako husema, “Njia ya Bwana haiko sawa!” lakini ni njia zako ndizo haziko sawa!
18Wakati mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye haki na kufanya dhambi, kisha atakufa katika hiyo!

19Wakati mtu mbaya ageukapo kutoka kwenye ubaya wake na kufanya iliyo halali na haki, ataishi kwa sababu ya hayo mambo!
20Lakini ninyi watu husema, “Njia ya Bwana haiko sawa!” Nitawahukumu kila mmoja wenu kulingana na njia yake, nyumba ya Israeli!”'
21Ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, siku ya tano ya mwezi wa kumi ya uhamisho wetu, mtu mmoja akatoroka kutoka Yerusalemuna kusema, “Mji umetekwa!”
22Mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu jioni kabla yule mtoro hajaja, na mdomo wangu ulikuwa wazi mda huo alikuja kwangu wakati wa mapambazuko. Hivyo mdomo wangu ulikuwa wazi; sikuwa bubu tena!
23Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
24“Mwanadamu, wale waishio mahali palipoharibika katika nchi ya Israeli huongea na kusema, 'Ibrahimu alikuwa mtu pekee, na alirithi nchi, lakini sisi tukowengi! Tumepewa nchi kama wamiliki.”
25Kwa hiyo waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Mnakula damu, na mmeziinulia macho yenu sanamu, kisha mnazimwagia damu za watu. Je! mna uhakika wa kuimiliki hii nchi?
26Mnategemea upanga wenu na mmetenda mambo maovu; kila mtu amemnajisi mke wa jirani yake. Je! kweli mtaimiliki nchi?'
27Utawaambia hivi, 'Bwana Yahwe asema hivi: Kama niishivyo, hakika wale walio katika uharibifu wataanguka kwa upanga, na nitawapatia wale walio katika mashamba viumbe hai kama chakula, na wale walio katika ngome na mapango watakufa kwa tauni.
28Kisha nitairudisha nchi kwenye ukiwa na tishio, na kiburi cha uwezo wake kitakoma, kwa kuwa milima ya Israeli itakuwa jangwa, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayewapitia.'
29Hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapoifanya nchi ukiwa na tishio kwa sababu ya machukizo yote waliyoyafanya.
30Hivyo basi wewe, mwanadamu-watu wako wanasema mambo yako karibu na kuta na malango ya nyumba, na kila mmoja anaambizana na mwenzake-kila mtu na ndugu yake, 'Twende na tukasikilize neno la nabii lililotoka kwa Yahwe!
31Hivyo watu wangu watakuja kwako, kama wafanyavyo mara nyingi, na nitaketi mbele yako na kusikiliza maneno yako, lakini mioyo yao inafuata udhalimu kwa faida yao.
32Kwa kuwa umekuwa kama wimbo mzuri kwao, sauti nzuri awezaye kucheza kinanda vizuri, hivyo watasikia maneno yako, lakini hakuna atakaye yatii.
33Hivyo wakati haya yote yatakapotokea-tazama! itatokea! -watajua yakwamba nabii alikuwa miongoni mwao.”