Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Neno la Yahwe likanijia tena, kusema,
2“Je mnamaana gani, ninyi mliotumia hii mithali kuhusiana na nchi ya Israeli na kusema, 'Wababa wamekula zabibu mbichi, na meno ya watoto imetiwa ganzi'?
3Kama nishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-bila shaka hakutakuwa na fursa yoyote tena kwa ajili yenu kuitumia hii mithali katika Israeli.
4Tazama! Kila uhai ni mali yangu-uhai wa baba na uhai wa mwana pia, ni mali yangu! roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa!
5Itasemwaje kuhusu mtu mwenye haki na achukuaye yaliyo halali na haki-
6kama asipokula juu ya milima au kuinua macho yake kwa sananmu za nyumba ya Israeli, na hakumnajisi mke wa jirani yake, wala kumsemesha mwanamke katika kipindi chake cha mwezi, je! Yu mwenye haki?
7Je! Itasemwaje kuhusu mtu ambaye hakumkandamiza yeyote, na kumrudisha mdeni wake kwa kile kilichokuwa kimewekwa kwa ajili ya rehani, na hakuiba lakini kuwapatia chakula wenye njaa na kuwafunika uchi kwa nguo, je yu mwenye haki?
8Je! Itasemwaje kuhusu mtu ambaye hakuchukua faida kubwa kwa ile pesa aliyokopa, na hakuchukua faida kubwa kwa kile alichokiuza?
9Amesemwa kwamba amechukua yaliyo halali na kuimarisha uaminifu kati ya watu. Kama huyo mtu akitembea katika sheria zangu na kuzishika hukumu zangu kufanya kwa uaminifu, kisha ahadi kwa ajili ya mtu mwenye haki ni hii: Ataishi hakika! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
10Lakini akizaa mwana mnyang'anyi mmwaga damu na kufanya mengi katika haya mambo kama yalivyotajwa hapa,
11hata kama baba yake hakufanya mojawapo katika haya mambo, lakini akala juu ya milima na akamnajisi mke wa jirani yake, Je! itasemwaje juu yake?
12Huyu mtu huwakandamiza maskini na wahitaji, na huwakamata na kuwanyang'anya, na hawarudishii dhamana, na huyanua macho yake kwa sanamu na kufanya matendo maovu,
13na hukopesha pesa kwa faida ya juu sana na kufanya faida kubwa juu ya anachokiuza, Je! huyo mtu ataishi? Hakika hataishi! Atakufa hakika na damu yake itakuwa juu yake kwa sababu amefanya haya mambo ya chuki.
14Lakini Tazama! tuseme kuna mtu aliyezaa mwana, na mwana wake huona dhambi zote za baba yake alizozifanya, na kupitia kuziona, hakuyafanya hayo mambo.
15Huyo mwana hakula juu ya milima, na hakuinua macho yake kwa sanamu za nyumba ya Israeli, na hakumtia unajisi mke wa jirani yake, Je! itasemwaje juu yake?
16Yule mwana hakumkandamiza yeyote, au kutwaa dhamana, au kupoteza vitu, lakini badala yake kutoa chakula chake kwa wenye njaa na kuwafunika wenye uchi kwa nguo.
17Huyo mwana hakumkandamiza yeyote au au kuchukua faida ambayo ni ya juu sana au kufanya manufaa kwa ajili ya mkopo, lakini ameyashika maagizo yangu na kuenenda sawa sawa na sheria zangu; huyo mwana hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake: Ataishi hakika!
18Baba yake, kwa kuwa aliwakandamiza wengine kwa nguvu nyingi na kumnyang'anya ndugu yake, na kufanya yasiyo mema miongoni mwa watu wake-tazama, atakufa katika uovu wake.

19Lakini ninyi husema, 'Kwa nini mwana asibebe uovu wa baba yake?' Kwa sababu mwana hubeba yaliyo halali na haki na kuzitunza amri zangu; huzifanya. Ataishi hakika!
20Yule atendaye dhambi, ndiye ambaye atakufa. Mwana hatabeba uovu wa baba yake, na baba hatabeba uovu wa mwana wake. Haki ya yule atendaye haki itakuwa juu yakwe mwenyewe, na uovu wa mwenye uovu utakuwa juu yake mwenyewe.
21Lakini kama mwovu ageukapo kutoka dhambi zake zote alizofanya, na kuzitunza sheria zangu zote na kufanya yaliyo halali na haki, kisha hakika ataishi na hatakufa.
22Makosa yote aliyoyafanya hayatakumbukwa juu yake. Ataishi kwa hiyo haki aliyoitenda.
23Je! Nitafurahia juu ya kifo cha mwovu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na sio katika kugeuka kwake kutoka njia yake ili kwamba aweze kuishi?
24Lakini kama mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye haki yake na kufanya maovu na kutenda machukizo kama machukizo yote ambayo mtu mwovu afanyayo, basi ataishi? Haki yake yote aliyoifanya haitakumbukwa wakati atakaponisaliti katika uhaini wake. Hivyo atakufa katika dhambi alizofanya.
25Lakini ninyi husema, 'Njia ya Bwana si sawa!' sikilizeni, nyumba ya Israeli! Je njia zangu haziko sawa? Je si njia ambazo haziko sawa?
26Wakati mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye makosa yake, na kufanya maovu na kufa kwa sababu ya hayo, kisha atakufa katika uovu ambao alioufanya.
27Lakini wakati mtu mwovu ageukapo kutoka uovu wake alioufanya na kufanya yaliyo halali na haki, kisha ataulinda uhai wake.
28Kwa kuwa ameona na kugeuka kutokana na makosa yake yote ambayo aliyoyafanya. Hakika ataishi, na hatakufa.
29Lakini nyumba ya Israeli husema, 'Njia ya Bwana haiko sawa!' Ni namna gani njia zangu si sawa, nyumba ya Israeli? Ni njia zenu ndizo si sawa.
30Kwa hiyo nitamuhukumu kila mtu miongoni mwenu kulingana na njia zake, nyumba ya Israeli! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. Tubuni na rudini kutoka kwenye makosa yenu yote ili kwamba wasiwe kikwazo cha uovu dhidi yenu.
31Tupilia mbali makosa yenu yote mliyoyafanya; jifanyieni moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, nyumba ya Israeli?
32Kwa kuwa sifurahii kifo cha yule afaye-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-hivyo tubuni na muishi!”