Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 5

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1“Kisha wewe mwana wa adamu, chukua upanga mkali kama wembe wa kinyozi kwa ajili yako mwenyewe, na pitisha hayo makali juu ya kichwa chako na ndevu zako, kisha chukua mizani za kupimia uzito na uzigawanye nywele zako.
2Choma theluthi ya tatu ya hiyo kwa moto katikati ya mji wakati siku za kuzingirwa zitakapokamilika, na chukua theluthi ya nywele na uipige kwa panga na kuuzunguka mji. Kisha tawanya theluthi yake kwenye upepo, na nitasogeza panga karibu ili kufukuza watu.
3Lakini chukua kiasi kidogo cha nywele na zifunge kwenye pindo za nguo yako.
4Kisha chukua tena zile nyewele na zitupe katikati ya moto; na zichome kwenye moto; kutoka hapo utatoka nje kwenda nyumba zote za Israeli.”
5Bwana Yahwe asema hivi, “Hii ndio Yerusalemu katikati ya mataifa, nilipomuweka, na ambapo nilipomzunguka kwa nchi zingine.
6Lakini anaudhaifu wa kukataa amri zangu zaidi kuliko mataifa yalivyo, na sheria yangu zaidi kuliko mataifa ambayo yanayomzunguka. Watu wamezikataa humuku zangu na kuacha kutembea katika sheria zangu.”
7Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, “Kwa sababu mmekuwa kikwazo kuliko mataifa ambayo yanayowazunguka na kuacha kutembea kwenye amri zangu wala kutenda kulingana na amri zangu, wala hata kutenda kulingana na amri za mataifa yanayowazunguka,”
8kwa hiyo Bwana asema hivi, “Tazama! Mimi mwenyewe nitatenda juu yenu. Nitato hukumu kati yenu ili mataifa waone.
9Nitawafanyia yale ambayo sijawahi kuyafanya na kile ambacho sintokifanya tena, kwa sababu ya matendo yenu ya kuchukiza.
10Kwa hiyo baba watawala watoto kati yenu, na watoto watawala baba zao, kwa kuwa nitafanya hukumu juu yenu na kuwatawanya kila mahali wote ninyi mliobaki.
11Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-bila shaka hii ilikuwa kwa sababu umapanajisi patakatifu pangu kwa mambo ya machukizo yako yote na kwa matendo yako yote niyachukiayo, kwamba mimi mwenyewe nitakupunguza katika hesabu; jicho langu halitakuhurumia, na sintoacha kukuharibu.
12Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na wataliwa na njaa katikati yenu. Theluthi wataanguka kwa upanga likiwazunguka. Kisha nitawatawanya theluthi katika mahali pote, na nitafuatisha upanga kuwafukuza pia.
13Hivi ndivyo ghadhabu yangu itavyokamilika, na nitasababisha ghadhabu yangu juu yao hata kulala. Nitajiridhisha, na watajua kwamba, mimi Yahwe, nimenena kwa ghadhabu yangu wakati nitakapo kamilisha ghadhabu yangu dhidi yao.
14Nitakufanya mkiwa kwa mataifa yanayokuzunguka kwenye uso wa kila mtu apitaye karibu.
15Hivyo Yerusalemu itakuwa jambo kwa watu wengine kushutumu na kufanya mzaha, na chukizo kwa mataifa ambayo yanayowazunguka. Nitafanya hukumu dhidi yenu kwa ghadhabu na hasira, na kwa kukemea kwa hasira-Mimi, Yahwe nimesema hivi!
16Nitatuma mishale mikali ya njaa juu yenu ambayo itakuwa na maana ya kwamba nitawaharibu. Kwa kuwa nitaongeza njaa juu yenu na kuvunja tegemeo lenu la mkate.
17Nitaleta njaa na majanga dhidi yenu hivyo mtakuwa wagumba. Tauni na damu zitapita kati yako, na nitaleta upanga dhidi yenu-Mimi Yahwe, nimesema hivi.”