Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 47

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha yule mtu akanirudisha nyuma kwenye lango la kuingia la hekalu, na kulikuwa na maji yakitiririka nje kutoka chini ya hekalu kizingiti cha nyumba kuelekea masharikii-kwa mbele ya hekalu kulekea mashariki-na maji yalikuwa yakitiririka chini upande wa kusini mwa hekalu, kuelekea upande wa kuume wa madhabahu.
2Hivyo akanileta kwenye lango la kaskazini na kuniongoza kuzunguka lango kuelekea mashariki, na hapo maji yalikuwa yakitiririka kutoka lango hili kwa upande wa kusini yake.
3Yule mtu alipokuwa akienda mashariki, kulikuwa na kamba ya kupimia kwenye mkono wake; akapima dhiraa elfu moja akanivusha kwenye maji hata maji yakafika kwenye magoti.
4Kisha akapima dhiraa elfu moja ten akanivusha kwenye yale maji yaliyofika kwenye magoti; akapima dhiraa elfu kumi nyingine na kunivusha maji yakafika hata kwenye nyonga.
5Tena akapima dhiraa elfu moja nyingine, lakini ulikuwa mto ambao sikuweza kuuvuka kwa sababu maji yalizidi na yalijaa maji ya kuogelea ndani-yalikuwa mto usiovukika
6Yule mtu akanambia, “Mwanadamu, unaona hii?” akanipeleka na kunirudisha karibu na ukingo wa mto.
7Nilipokuwa nikirudi, hapo kwenye ukingo wa mto kulikuwa na miti mingi katika huu upande na upande mwingine pia.
8Yule mtu akanambia, “Haya maji yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki na chini hata Araba; haya maji hutiririka kwenye Bahari ya Chumvi itaifanya kuwa mpya.
9Itakuwa kwamba kila kiumbe hai kisongamanacho kitaishi mahali maji yanapoelekea; kutakuwa na samaki wengi, kwenye hayo maji yatiririkayo huko. Itafanya maji ya chumvi kuwa mapya. Kila kitu kitaishi popote mto utakapoelekea.
10Kisha itatokea kwamba wavuvi wa En Gedi watasimama karibu na maji, na kutakuwa na sehemu ya kutandazia nyavu za samaki karibu na En Eglaimu. Kutakuwa na samaki nyingi za aina tofauti tofauti katika Bahari ya Chumvi, kama samaki kwenye Bahari Kuu kwa wingi wao.
11Lakini Bahari ya Chumvi ikajaa maji na matope hayataachwa mapya; yataachwa yawe kwa ajili ya kutengeneza chumvi.
12Karibu na huo mto juu ya ukingo wake, pande zote, aina zote za miti utazaa chakula. Majani yake hayatanyauka na matunda yake hayataacha kukua. Kila mwezi miti itazaa matunda, kwa sababu maji kutoka patakatifu yatatirirka kwenda kwenye hiyo miti. Matunda yake yatakuwa kwa ajili ya chakula, na majani yake yatakuwa kwa ajili ya dawa.
13Bwana Yahwe asema hivi: Hii itakuwa njia ambayo mtaigawanya nchi kwa ajili ya kabila kumi na mbili za Israeli: Yusufu atakuwa na mafungu mawili.
14Mtaigawa kila mtu sawa sawa ambayo niliinua mkono wangu na kuapa kuwapa baba zenu. Hii nchi itakuja kuwa urithi kwenu.
15Huu utakuwa mpaka wa nchi upande wa kaskazini kutoka Bahari Kubwa kwa njia ya Hethloni, na kisha kuelekea Zedada.
16Kisha mpaka utaenda hata Berotha, hadi Sibraimu, iliyopo kati ya Damaskasi na Hamathi, na kisha hata Hazer-hatikoni, iliyopo karibu na mpaka wa Haurani.
17Hivyo mpaka utaenda kutoka kwenye bahari hadi Hazar-enoni kwenye mpaka wa Damaskasi na Hamathi hata kaskazini. Huu utakuwa upande wa kaskazini.
18Kwa upande wa mashariki, kati ya Haurani na Damaskasi na kati ya Geliadi na nchi ya Israeli kutakuwa na mto Yordani. Mtapima kutoka kwenye mpaka hata kwenye bahari ya mashariki; huo wote utakuwa mpaka wa mashariki.

19Kisha upande wa kusini: kusini mwa Tamari hadi kwenye maji ya Meriba Kadeshi, kijito cha Misri hata Bahari Kuu, na upande wa kusini kuelekea kusini.
20Kisha mpaka wa magharibi utakuwa Bahari Kuu utaelekea hata nyuma ya Hamathi. Huu utakuwa upande wa mgharibi.
21Kwa njia hii mtaigawanya hii nchi kwa ajili yenu wenyewe, kwa kabila za Israeli.
22Hivyo mtagawana urithi kwa ajili yenu wenyewe na kwa ajili ya wageni walio kati yenu, wale watakaozaa watoto kati yenu na waliokuwa, kati yenu, kama wazaliwa wa watu wa Israeli. Mtapewa urithi miongoni mwa makabila ya Israeli.
23Kisha itatokea kwamba wageni watakuwa pamoja na kabila miongoni mwa yule anayeishi. Mtapatia urithi-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”