Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 38

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Neno la Yahwe likanijia, likisema,
2“Mwanadamu, weka uso wako kumwelekea Gogu, nchi ya Magogu, kiongozi mkuu wa Mesheki na Tubali; na kutabiri dhidi yake.
3Sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako, Gogu, kiongozi mkuu wa Mesheki na Tubali.
4Hivyo nitakugeuza na kuweka kulabu kwenye taya yako; nitakupeleka nje pamoja na jeshi lako lote, farasi, na waendesha farasi, wote wakiwa wamevaa silaha, kusanyiko kubwa pamoja na ngao ndogo na ngao kubwa, wote wakishikilia panga!
5Persia, Kushi, Uajemi wapo pamoja nao, wote pamoja na ngao na chapeo!
6Gomeri na jeshi lake lote, na Beth-Togarma, kutoka sehemu za mbali ya kaskazini, na jeshi lake lote! Watu wengi wako pamoja nawe!
7Kuwa tayari! Ndio, jiandae na jeshi lako waliokusanyika pamoja na wewe, na amiri wao mkuu.
8Utaitwa baada ya siku nyingi, na baada ya miaka michache utaenda kwenye nchi iliyofunikwa kutoka upanga na ambayo iliyokusanywa kutoka watu wengi, iliyowkusanya kuwarudisha milima ya Israeli ambayo imeendelea kuangamizwa. Lakini watu wa nchi watatolewa na kabila za watu, na wataishi salama, wote!
9Hivyo utapanda juu kama tufani iendavyo; utakuwa kama wingu lililofunika nchi, wewe na jeshi lako lote, maaskari wako wote pamoja na wewe.
10Bwana Yahwe asema hivi: Itakuwa siku hiyo hayo mawazo yataingia moyoni mwako, na utatunga njama mbaya.'
11Kisha utasema, 'nitapanda hata nchi iliyowazi; nitaenda hata kwa watu wapole waishio salama, wote wakiishi mahali ambapo hakuna kuta wala makomeo, na mahali ambapo hakuna malango ya mji.
12Nitanyakua mateka na kuiba mateka, ili nilete mkono wangu juu kuwaangamiza wale wakazi wapya, na juu ya watu waliokusanyika kutoka mataifa, watu wale waongezao wanyama na mali, na wale waishio katikatika ya dunia.'
13Sheba na Denani, na wafanya biashara wa Tarshishi pamoja na mahodari wake wote watakwambia, 'Je, umekuja kuteka nyara? Je, umewakusanya majeshi yako kuchukua mateka, kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua mifugo yao na mali na kuwakokota mateka wengi sana?'
14Kwa hiyo tabiri, mwanadamu, na mwambie Gogu, 'Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku hiyo, wakati watu wangu Israeli watakapoishi salama, je, hutajifunza kuhusu wao?
15Utakuja kutoka mahali pangu mbali katika kaskazini pamoja na jeshi kubwa, wote wakiendesha farasi, kusanyiko kubwa, jeshi kubwa.
16Utawashambulia watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Katika siku za baadaye nitakuleta juu ya nchi yangu, ili mataifa wanijue nitakapojifunua mwenyewe kupitia wewe, Gogu, kuwa mtakatifu mbele ya macho yao.
17Bwana Yahwe asema hivi: Je, wewe siye yule ambaye niliyeongea naye katika siku za zamani kwa mkono wa watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri katika mda wao wenyewe kwa miaka niliyowaleta juu yao?
18Basi itakuwa katika siku hiyo wakati Gogu atakapo ishambulia nchi ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-ghadhabu yangu itapanda katika hasira yangu.

19Katika wivu wangu katika hasira ya moto wangu, ninasema kwamba katika siku hiyo kutakuwa na tetemeko kubwa la nchi katika nchi ya Israeli.
20Watatetemeka mbele yangu-samaki wa baharini na ndege wa angani, wanyama wa mashambani, na viumbe watambaao juu ya nchi, na kila mtu aliyeko juu ya uso wa nchi. Milima itaangushwa chini majabali yataanguka, hadi kila ukuta utaanguka kwenye nchi.
21Nitaita upanga dhidi yake juu ya milima yangu yote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-upanga wa kila mtu utakuwa kinyume na ndugu yake.
22Kisha nitamuhukumu kwa tauni na damu; nakufurika mvua na mvua ya mawe na kuchoma asidi nitainyeshea chini juu yake na jeshi lake na mataifa mengi yaliyo pamoja naye.
23Kwa kuwa nitaonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu na nitafanya kujulikana mimi mwenyewe katiaka macho ya mataifa mengi, na watajua kwamba mimi ni Yahwe.”